-
Iran yatoa mkono wa pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais Magufuli
Mar 20, 2021 01:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za mkono wa pole kwa wananchi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli.
-
Qalibaf: Ni lazima Marekani iondoe vikwazo vyote dhidi ya Iran
Mar 19, 2021 08:48Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema: "Marekani inapaswa kuondoa vikwazo vyote ili Iran iweze kutekeleza ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA."
-
Khatibzadeh: Saudia imeliteka nyara Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi
Mar 19, 2021 04:35Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran usiku wa kuamkia leo amejibu taarifa ya mwisho ya kikao cha hivi karibuni cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na kusema kuwa utawala wa kiimla wa Saudi Arabia umeliteka nyara baraza hilo na unachochea chuki na machafuko katika eneo hili kupitia kutwisha kwake misimamo yake isiyokubalika.
-
Nguvu za SEPAH za kukabiliana na Marekani na Israel zinaongezeka siku baada ya siku
Mar 18, 2021 23:22Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, jeshi hilo limejikita kwenye kuongeza nguvu zake za kukabiliana na mikakati ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran: Ulimwengu wa Kiislamu una wajibu wa kupambana vilivyo na misimamo mikali
Mar 18, 2021 03:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ulimwengu wa Kiislamu una wajibu wa kupambana vilivyo misimamoo mikali ndani yake. Amesema, ni wajibu wa ulimwengu huo kuunganisha nguvu zake kupambana na watu wenye aidiolojia za chuki na za kuwakufurisha Waislamu wengine.
-
Chanjo za corona zilizotengenezwa Iran karibu zitaanza kutumika katika soko la ndani
Mar 17, 2021 23:23Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran ametangaza kuwa chanjo za corona zilizotengenezwa nchini karibu zitaanza kutumika katika soko la ndani.
-
Iran yaadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Imam Hussein (AS)
Mar 17, 2021 04:03Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeungana na ulimwengu wa Kiislamu hii leo kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume wetu mtukufu Muhammad (SAW).
-
Iran yakosoa undumakuwili wa Uingereza, yataka silaha zote za nyuklia ziharibiwe
Mar 17, 2021 03:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali undumakuwili wa Uingereza; ambayo kwa upande mmoja inatoa madai yasiyo na msingi dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani na kwa upande mwingine, inasema kuwa inataka kuongeza akiba ya silaha zake za nyuklia.
-
Iran yakanusha kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani
Mar 17, 2021 01:00Duru za kiusalama nchini Iran zimekadhibisha madai ya Marekani kwamba kuna mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yanayoendelea baina ya Tehran na Washington.
-
Rouhani: Kufidia makosa yaliyofanywa na serikali iliyopita ya Marekani ni kwa manufaa ya wote
Mar 16, 2021 09:01Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kufidia makosa yaliyofanywa na serikali iliyopita ya Marekani si kwa manufaa ya Iran tu bali ni kwa maslahi ya Marekani yenyewe , eneo na taasisi za kimataifa.