Iran: Ulimwengu wa Kiislamu una wajibu wa kupambana vilivyo na misimamo mikali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68022-iran_ulimwengu_wa_kiislamu_una_wajibu_wa_kupambana_vilivyo_na_misimamo_mikali
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ulimwengu wa Kiislamu una wajibu wa kupambana vilivyo misimamoo mikali ndani yake. Amesema, ni wajibu wa ulimwengu huo kuunganisha nguvu zake kupambana na watu wenye aidiolojia za chuki na za kuwakufurisha Waislamu wengine.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 18, 2021 03:44 UTC
  • Iran: Ulimwengu wa Kiislamu una wajibu wa kupambana vilivyo na misimamo mikali

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ulimwengu wa Kiislamu una wajibu wa kupambana vilivyo misimamoo mikali ndani yake. Amesema, ni wajibu wa ulimwengu huo kuunganisha nguvu zake kupambana na watu wenye aidiolojia za chuki na za kuwakufurisha Waislamu wengine.

Dk Mohammad Javad Zarif amesema hayo katika kikao cha jana Jumatano cha ngazi za juu cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kilichofanyika kwa njia ya Intaneti mjini New York Marekani, kwa ajili ya kuchunguza chuki dhidi ya Uislamu zinazoenezwa ulimwenguni.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alikuwa mzungumzaji wa kwanza na alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika suala zima la chuki zinazoenezwa dhidi ya Uislamu na wajibu wa dunia nzima kupambana vikali na jambo hilo.

Bendera za wanachama wa OIC

 

Katika hotuba hiyo, Dk Zarif amesisitizia wajibu wa kutekelezwa ipasavyo malengo ya OIC likiwemo suala zima la Waislamu wa madhehebu yote kuishi pamoja kwa usalama na amani na kuhamasisha mazungumzo yenye manufaa katika ulimwengu wa Kiislamu na baina ya dini na tamaduni tofauti duniani.

Ameongeza kuwa, chuki dhidi ya wageni, dhuki dhidi ya Uislamu, misimamo mikali, taasubu za kimadhehebu, kuendelea kuongezeka ukosefu wa uadilifu na watu wa jamii nyingine kushindwa kuvumilia kuishi na Waislamu na kufanyiwa ukandamizaji wa kila namna Waislamu wa maeneo mbalimbali duniani, zilikuwa ni miongoni mwa mambo muhimu ya kushughulikiwa vilivyo leo hii duniani.