-
Kiongozi Muadhamu: Mab’ath ni sikukuu ya wapigania uadilifu kote ulimwenguni
Mar 11, 2021 09:27Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, sikukuu kubwa ya Mab’ath na kumbukumbu ya kubaathiwa na kupewa Utume Mtume Muhammad SAW ni ya wapigania uadilifu kote ulimwenguni.
-
Rais Rouhani: Taifa la Iran limeibuka mshindi katika vita vya irada
Mar 11, 2021 04:37Rais Hassan Rouhani amesisitiza kuwa kuibuka mshindi taifa la Iran katika vita vya irada kumewafanya watawala wa Ikulu ya White House wakiri mara kadhaa kushindwa kwa vita na mashinikizo yao ya juu kabisa.
-
Rouhani amueleza Johnson: Kama tunataka diplomasia, njia iko wazi; Marekani iondoe vikwazo na kutekeleza majukumu yake
Mar 10, 2021 23:57Rais Hassan Rouhani amesema Marekani ndiye mkiukaji mkubwa wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa; na sambamba na kusisitiza kuwa haifai kukihamasisha kitendo hicho au kukiacha bila kukichukulia hatua, amesema: Kama tunataka kutumia diplomasia, njia yake iko wazi; ni kuondolewa vikwazo, na Marekani kutekeleza majukumu yake; na hakuna chaguo jengine lolote lile.
-
Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran: Bwabwaja za Wazayuni chimbuko lake ni woga
Mar 10, 2021 21:20Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, bwabwaja na uropokaji wa Wazayuni unatokana na woga na hofu walionayo, kwani wafahamu vyema uwezo ulionao mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Rouhani: Wazayuni wanataka vikwazo dhidi ya Iran viendelee
Mar 10, 2021 08:37Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Wazayuni na watawala wasiotaka mageuzi katika eneo wanataka vikwazo vya kidhalimu dhidi ya watu wa Iran viendelee.
-
Salehi: Fatwa ya Kiongozi Muadhamu ya uharamu wa bomu la Atomiki, ndio msimamo usiobadilika wa Iran
Mar 10, 2021 03:46Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, fatwa ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu uharamu wa bomu la atomiki ndio msimamo usiobadilika wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu silaha hizo angamizi.
-
Iran: Ni sisi tu undio tuliotekeleza mapatano ya nyuklia ya JCPOA
Mar 10, 2021 03:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia jinsi nchi za Ulaya na Marekani zilivyoshindwa kutekeleza mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kuwa, ni Iran pekee ndiyo iliyotekeleza makubaliano hayo ya kimataifa.
-
Rais Rouhani: Njia pekee bora ya kuyakurubisha pamoja mataifa ya dunia ni kujiimarisha kielimu na kiutamaduni
Mar 09, 2021 23:19Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia pekee ya kudumu kwa ajili ya kuyafanya mataifa ya dunia yakurubiane zaidi, ni kujiimarisha kielimu na kiutamaduni.
-
Kiongozi Muadhamu: Wanawake mashahidi, majeruhi wa vita; ni vilele bora vya fakhari za Mapinduzi ya Kiislamu
Mar 09, 2021 09:14Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu kwa Kongamano la Taifa la "Jeshi la Malaika Walioweka Historia" lililoitishwa maalumu kwa ajili ya kuwaenzi wanawake waliouawa shahidi, majeruhi wa vita na walioachiliwa huru na kusema kuwa, wanawake hao wanamapambano na mashujaa wenye kujitolea katika njia ya haki, ni vilele bora vya fakhari za Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Iran itakuwa mzalishaji mkubwa wa chanjo
Mar 09, 2021 08:42Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, hivi karibuni Iran itakuwa mzalishaji mkubwa wa chanjo ya COVID-19 duniani.