-
Iran: Trump ameenda, Ghuba ya Uajemi imebakia; alishindwa kutuzuia kuuza mafuta yetu
Jan 22, 2021 08:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari wakati wote kwa ajili ya mazungumzo na nchi nyingine za Ghuba ya Uajemi kwa ajili ya kulinda usalama na kudumisha amani na ushirikiano katika eneo hili.
-
Zaidi ya wagonjwa milioni 1 na laki 1 na 51,000 wapata afueni ya COVID-19 nchini Iran
Jan 22, 2021 08:22Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, zaidi ya wagonjwa milioni 1 na laki 1 na 51 elfu wa COVID-19 wamepata afueni nchini Iran.
-
Catherine Ashton: Baada ya Iran kupata ushindi dhidi ya Trump, haitasalimu amri
Jan 22, 2021 04:50Catherine Ashton, Mkuu wa zamani wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema katika makala ya pamoja na Chuch Hagel, Waziri wa Zamani wa Ulinzi wa Marekani kwamba, Washington inapaswa kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Abdolahian: Kipimo cha wananchi wa Iran ni vitendo vya viongozi wapya wa Marekani, si maneno
Jan 22, 2021 00:26Msaidizi Maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amegusia kuingia madarakani serikali mpya nchini Marekani na huku akisisitiza kwamba hivi sasa mapatano ya JCPOA yamebakia jina tu amesema, kipimo cha wananchi wa Iran ni vitendo vya viongozi wapya huko White House.
-
Iran yakaribisha wito wa kufanyika mazungumzo kwa ajili ya kuleta amani na maelewano katika eneo
Jan 21, 2021 23:01Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote imekuwa ikisisitiza udharura wa kufanyika mazungumzo na kuheshimiana mataifa ya eneo la Asia Magharibi na hasa Ghuba ya Uajemi na kutangaza wazi hamu yake ya kutaka kuwa na uhusiano mzuri na wa kimantiki na majirani zake wote.
-
Zarif: Mjumbe wa Iran UN hajazungumza na Marekani
Jan 21, 2021 00:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa hajafanya mazungumzo yoyote na Marekani kama lilivyodai gazeti moja la Ufaransa.
-
Misimamo ya maafisa wa serikali ya Biden kuhusu Iran; kurudiwa misamiati ile ile ya zamani
Jan 20, 2021 23:40Sherehe za kutawazwa Joseph Robinette Biden Jr. kuwa rais wa 46 wa Marekani zimefanyika katika hali ambayo, Jumanne, tarehe 19 Januari 2021, maafisa wa ngazi za juu wa serikali yake walitumia kikao cha Baraza la Sanate la nchi hiyo kutangaza misimamo yao kuhusu Tehran na masuala yanayohusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rouhani: Washington imegeuzwa kuwa kambi ya kijeshi katika siku ya kuapishwa Biden
Jan 20, 2021 08:49Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa leo ni siku ya kufikia ukomo wa utawala wa Donald Trump na kueleza kuwa Washington imgeuzwa kuwa kambi ya kijeshi katika siku ya kuapishwa rais mpya wa Marekani.
-
Zarif: Muqawama wa Wairani umefelisha mashinikizo ya juu ya Marekani
Jan 19, 2021 23:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema muqawama, mapambano na kusimama kidete wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu kumeipigisha mweleka sera ya mashinikizo ya juu kabisa ya Marekani dhidi ya taifa hili.
-
Tehran mwenyeji wa mkutano kwa njia ya video wa mabunge yanayounga mkono Quds na Palestina
Jan 19, 2021 07:09Jumatatu ya jana tarehe 18 Januari, mji mkuu wa Iran Tehran ulikuwa mwenyeji wa mkutano uliofanyika kwa njia ya mawasiliano ya intaneti chini ya anuani ya "Gaza; nembo ya muqawama" wa mabunge yanayoiunga mkono Quds na Palestina.