-
Zaidi ya wagonjwa 4,000 wapya wa corona wagunduliwa Iran; vifo vipya 239 vyaripotiwa
Oct 07, 2020 09:00Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran ametangaza kuwa, zaidi ya wagonjwa wapya elfu 4,000 wa COVID-19 wamegunduliwa humu nchini katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na wagonjwa 239 wamefariki dunia katika muda huo.
-
Mfumo wa kisasa wa rada wa Qadiir wazinduliwa, mafanikio mapya ya sekta ya ulinzi ya Iran
Oct 07, 2020 07:42Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kukidhi zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji yake ya zana za kujilinda licha ya vikwazo na vizingiti vingi ilivyowekewa.
-
Iran iko tayari kusaidia utatuzi wa mgogoro baina ya Jamhuri ya Azerbaijan na Armenia
Oct 07, 2020 01:18Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mgogoro baina ya Armenia na Jamhuri ya Azerbaijan unapaswa kumalizika haraka iwezekanavyo. Ameongeza kuwa, Iran iko tayari kuchukua hatua yoyote ya kutatua mgogoro baina ya Baku na Yerevan kwa mujibu wa sheria za kimataifa na mipaka inayotambuliwa rasmi ya nchi hizo mbili.
-
Iran yazindua kizazi kipya cha mfumo wa rada wa Qadir
Oct 07, 2020 01:17Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limezindua kizazi kipya cha mfumo wa rada wa ulinzi wa anga uliopewa jina la Qadir ambao ni wa masafa marefu na unaotumia mfumo wa 3D.
-
Rouhani: Taifa la Iran halitarajii chochote kutoka Marekani isipokuwa uadui
Oct 06, 2020 08:47Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria miongo mtawalia ya uadui wa Marekani kwa taifa la Iran na kusema: Taifa la Iran halitarajii chochote kutoka Marekani isipokuwa uadui.
-
Udhaifu wa Ulaya wa kushindwa kuondoa vikwazo ilivyowekewa Iran kama ilivyokubalika katika JCPOA
Oct 06, 2020 04:43Baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kukiuka waziwazi makubaliano hayo, Iran ilichukua hatua, zaidi ya ilivyotarajiwa, kwa kuendelea kwa muda wa mwaka mzima kutekeleza kikamilifu majukumu yake katika makubaliano hayo.
-
Khatibzadeh: Saudia na Israel zinapasa kuwa za mwisho kabisa kuzungumzia faili la nyuklia la Iran
Oct 05, 2020 21:28Msemaji wa Wizara ya Mashaurio ya Kigeni ya Iran amesisitiza kuwa, Saudi Arabia na utawala haramu wa Israel zinapaswa kuwa za mwisho kabisa kuzungumzia faili la miradi ya nyuklia ya Tehran.
-
Nchi za Ulaya zimeshindwa kutumiza ahadi zao kwa Iran
Oct 05, 2020 06:04Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita, baada ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, nchi za Ulaya zimeonyesha wazi kuwa hazina uwezo wa kuondoa vikwazo dhidi ya Iran.
-
Iran ipo mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, lakini bila ya uungaji mkono wa kutosha wa kimataifa
Oct 05, 2020 05:57Katika miaka ya karibuni, Jamhuri ya Kiislamu pekee imegundua na kunasa asilimia 76 ya madawa ya kulevya aina ya afyuni, asilimia 67 ya morfini na asilimia 17 ya heroini ya kiwango chote kinachotumika duniani.
-
Zaidi ya tani 3 za mihadarati zakamatwa kusini mashariki mwa Iran
Oct 05, 2020 04:42Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi la mkoa wa Sistan na Baluchistan huko kusini mashariki mwa Iran ametangaza habari ya kukamatwa zaidi ya tani tatu za madawa ya kulevya mkoani humo.