-
Mamilioni washiriki maombolezo ya Tasua kwa kuchunga protokali za afya
Aug 29, 2020 03:32Licha ya janga la corona, na huku wakichunga protokali za afya, mamilioni ya Waislamu wa Iran na maeneo mengine ya dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 9 Mfunguo Nne Muharram wameshiriki katika vikao, majlisi na shughuli za maombolezo ya Tasua.
-
Zarif aipa Marekani somo la sheria baaada ya kubwagwa mara 3 katika UNSC
Aug 29, 2020 03:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kushangazwa kwake na kitendo cha Marekani cha kutishia tena kumwekea vikwazo mtu au taasisi yoyote inayoshirikiana na Iran, licha ya kupigwa mweleka mara tatu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Iran: Siasa za kujikumbizia kila kitu upande wake Marekani zaidhoofisha UN
Aug 28, 2020 22:39Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo ameandika kwenye ukurasa wa kijamii wa Twitter kwamba, siasa za Marekani za kujikumbizia kila kitu upande wake zinaudhoofisha Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo.
-
Iran: 'Mashariki ya Kati' mpya itaanzishwa kwa kutimuliwa Marekani katika eneo
Aug 28, 2020 08:05Msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Iran katika masuala ya kimataifa amesema: 'Mashariki ya Kati' mpya itaundwa baada ya kuhakikisha Marekani imeshatimuliwa kikamilifu katika eneo hili la Asia Magharibi.
-
Iran: Huwi tena gaidi ukishamlipa pesa Trump
Aug 27, 2020 06:51Mkurugenzi Mkuu wa Asia Magharibi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuhusu pendekezo lililotolewa na Marekani kwa Sudan la kuitaka ilipe dola milioni 330 ili jina la nchi hiyo liondolewe kwenye orodha ya ugaidi ya Washington kwamba: Huwi tena gaidi ukishamlipa pesa Trump.
-
Taarifa ya pamoja ya Tehran; nia njema ya Iran na matarajio ya Tehran kwa IAEA
Aug 27, 2020 05:12Baada ya mazungumzo ya kina ya siku mbili ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) mjini Tehran, Iran na wakala huo wamefikia makubaliano kuhusu namna ya kutatua masuala mbalimbali kwa nia njema.
-
Taarifa ya pamoja ya Iran na Wakala wa IAEA; Iran yaruhusu kufikiwa maeneo mawili maalumu
Aug 26, 2020 23:33Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) zimetoa taarifa ya pamoja mwishoni mwa safari ya siku mbili ya Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa wakala huo hapa Tehran na kufuatia mazungumzo kati yake na viongozi mbalimbali wa Iran.
-
Mazungumzo ya Grossi Tehran; tathmini chanya ya Iran na IAEA kuhusu mashirikiano yao
Aug 26, 2020 23:32Mashirikiano ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) yamekuwa siku zote yakifanyika kwa msingi wa kutekeleza majukumu ya kimataifa na kwa kufuata miongozo ya kiufundi na kitaalamu.
-
Rouhani: Taifa la Iran limetegemea utamaduni wa Ashura katika ushindi wake mkabala wa njama za adui
Aug 26, 2020 09:00Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia siku hizi za maombolezo na kukumbuka mauaji ya Imam Hussein AS, mjukuu wa Mtume Muhammad SAW na kusema: "Taifa la Iran limepata ushindi kwa kusimama kidete na kupambana na njama za madola makubwa, na ushindi huo umetokana na kufuata utamaduni wa Ashura."
-
Iran yaunga mkono utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Syria
Aug 26, 2020 08:33Mshauri wa ngazi za juu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kisiasa amekutana na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria na kusema Tehran inaunga mkono mchakato wa kutatua mgogoro wa Syria kwa njia sa kisiasa.