Iran yaunga mkono utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Syria
Mshauri wa ngazi za juu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kisiasa amekutana na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria na kusema Tehran inaunga mkono mchakato wa kutatua mgogoro wa Syria kwa njia sa kisiasa.
Ali Asghar Haji ameyasema hayo mjini Geneva alipokutana na kufanya mazungumzo na Geir Pedersen, mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria. Mkutano huo wa Geneva umefanyika kujadili matukio ya hivi karibuni nchini Syria hasa kikao maalumu cha tatu cha Kamati ya Katiba ya Syria.
Asghar Haji amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Syria na amesisitiza umuhimu wa kuendelezwa mazungumzo ya Kamati ya Katiba ya Syria.
Mjumbu maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria pia katika mkutano huo amepongeza nafasi ya Iran katika kuunga mkono Kamati ya Katiba ya Syria na kusema ameridishwa na matokeo ya siku ya kwanza ya mazungumzo ya kamati hiyo.
Halikadhalika Mshauri wa ngazi za juu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amefanya mahojiano na Televisheni ya Al Mayadeen na kusema katika KKamati ya Katiba ya Syria na mchakato wa amani wa Astana, nchi zote zilizo katika mchakato huo zinaafikiana kimtazamo.
Ameashiria uingiliaji wa Marekani katika utendaji wa Kamati ya Katiba ya Syria na kusema: "Uingiliaji wowote katika masuala ya Kamati ya Katiba ya Syria haukubaliki." Ameongeza kuwa Marekani haijawahi kuwa na nafasi chanya nchini Syria na imezidisha mgogoro wa nchi hiyo. Ameongeza kuwa, Marekani inawasaidia magaidi wa ISIS na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa, nchi za Ulaya ambazo daima zimekuwa zikiunga mkono mitazamo ya Marekani sasa zinajaribu kujiweka mbali na Washington.