-
Makamu wa Rais wa Iran: Ukatili wa polisi ya Marekani unatokana na fikra za kibaguzi
Aug 26, 2020 03:08Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ukatili wa polisi ya Marekani unatokana na chuki ya kihistoria yenye mizizi katika fikra ya ubaguzi wa rangi inayotawala nchi hiyo.
-
Zarif: Tunataka tuwe na uhusiano mzuri na IAEA
Aug 25, 2020 22:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA hapa nchini ilikuwa na mafanikio makubwa na kusisitiza kuwa, Tehran inataka kuwa na uhusiano wa kawaida na mzuri na wakala huo na kuonya kuhusu ukwamishaji mambo unaofanywa na maadui.
-
Salehi: Wakala wa IAEA unapaswa kufanya kazi zake kwa uhuru
Aug 25, 2020 07:28Mkuu wa Taasisi ya Atomiki ya Iran (AEOI) amesema kuwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) unapaswa kufanya kazi zake kwa uhuru na kusisitiza kuwa Iran haiko tayari kutekeleza masuala ambayo yako nje ya ahadi zake kimataifa.
-
Ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiulinzi baina ya Iran na Russia kufunguliwa
Aug 25, 2020 07:23Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, baada ya kumalizika vikwazo vya silaha dhidi ya Iran, kutafunguliwa ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiulinzi baina ya Tehran na Mascow.
-
Zarif aushangaa uchu wa Pompeo wa kurundika silaha za US Asia Magharibi
Aug 25, 2020 03:36Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemkosoa vikali Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kwa kuvunja sheria za nchi hiyo ili kukidhi uchu wake wa kutaka kuuza silaha za kijeshi kwa wingi katika nchi za eneo la Asia Magharibi.
-
Safari ya Rafael Grossi mjini Tehran; fursa ya kujenga upya hali ya kuaminiana kati ya Iran na IAEA
Aug 25, 2020 03:26Kwa kutegemea ripoti zilizotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ukaguzi mkali na wa kiwango cha juu zaidi katika historia ya wakala huo, ukiwemo ukaguzi kamili wa zaidi ya mara 30 kwa mwaka pamoja na ule wa kushtukiza kwa mujibu wa Protokali ya Nyongeza, umefanywa na wakaguzi wa IAEA katika vituo vya nyuklia vya Iran.
-
Spika Qalibaf: Mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa ya Marekani dhidi ya Iran hayajawa na mafanikio
Aug 24, 2020 23:09Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa ya Marekani dhidi ya Tehran hayajawa na natija ya maana na katika miezi na miaka ijayo hali ya uchumi ya taifa hili itabobereka zaidi.
-
Kuendelea ushirikiano baina ya Iran na Venezuela na shukrani za Maduro kwa Tehran
Aug 24, 2020 22:58Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa msaada wake kwa nchi hiyo katika kukabiliana na vikwazo vya mafuta vya Marekani dhidi ya Venezuela na kusisitiza kuwa, uzoefu wa Iran utaweza kuisaidia nchi yake kutia nguvu uwezo wake wake wa kujitawala.
-
Khatibzadeh: Makubaliano ya Imarati na Israel ni jeraha kwa Ulimwengu wa Kiislamu
Aug 24, 2020 08:43Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, makubaliano ya utawala wa Imarati na Israel ya kuanzisha uhusiano baina yao ni jeraha kwa Ulimwengu wa Kiislamu na Waislamju katu hawatasahau khiana na usaliti huu dhidi ya Quds.
-
Maulamaa wa Kisunni Iran walaani makubaliano ya Israel na UAE
Aug 24, 2020 07:31Wanazuoni wa Kisunni hapa nchini Iran wamekosoa vikali mapatano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya pande mbili hizo.