Aug 24, 2020 13:13 UTC
  • Khatibzadeh: Makubaliano ya Imarati na Israel ni jeraha kwa Ulimwengu wa Kiislamu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, makubaliano ya utawala wa Imarati na Israel ya kuanzisha uhusiano baina yao ni jeraha kwa Ulimwengu wa Kiislamu na Waislamju katu hawatasahau khiana na usaliti huu dhidi ya Quds.

Saeed Khatibzadeh, msemaji mpya wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo leo ambapo ameashiria kuanzishwa uhusiano baina na Imarati na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa, endapo eneo la Asia Magharibi litakabiliwa na tishio kutoka kwa utawala vamizi wa Israel, basi utawala wa Abu Dhabi ndio unaopaswa kubeba dhima ya hilo. 

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia uhusiano wa Tehran na nchi za Kiarabu na Kiislamu kufuatia harakati za baadhi ya watawala wa Kiarabu za kuanzisha uhusiano na Israel na kueleza kwamba, Tel Aviv imeonyesha kuwa haiwezi kujidhaminia usalama wake na hakuna ahadi na makubaliano ambayo Israel haikuyavunja kama ambavyo hakuna mauaji ambayo hayajafanywa na utawala huo ghasibu; huu ni uukweli ambao hauwezi kubadilika.

Hatua ya Imarati ya kufikia makubaliano ya kuanzisha uhusiano na Israel imeendelea kukosolewa katika kila kona ya dunia

Kuhusiana na safari ya Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) hapa Tehran, Saeed KKhatibzadeh amesema kuwa, uhusiano wa taifa hilo la wakala wa IAEA siku zote uumekuwa na umuhimu mkubwa ingawa katika miaka ya hivi karibunii umekuwa na hali ya panda shuka.

Tags