-
Zarif: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono mapambano ya Wapalestina
Aug 16, 2020 02:11Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumamosi usiku amefanya mazungumzo na Riyad al-Maliki Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono mapambano ya taifa la Palestina ili liweze kupata haki zake.
-
Kiongozi Muadhamu: Mapinduzi ya 1953 yalikuwa mwanzo wa uhasama wa Marekani dhidi ya Iran
Aug 16, 2020 02:06Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, uhasama wa Marekani dhidi ya Iran ulianza mwaka 1953 wakati ilipoangushwa serikali ya wakati huo ya Iran na kwamba uhasama huo ungali unaendelea hadi wakati huu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Raisi: Kuundwa mahakama ya kimataifa kutadhamini utekelezaji wa haki za binadamu za Kiislamu
Aug 15, 2020 21:48Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema, kuundwa mahakama ya kimataifa kutadhamini kutekelezwa haki za binadamu za Kiislamu; na akaongeza kuwa: Mahakama ya Kimataifa ya Kiislamu inapasa iwapandishe kizimbani na kuwahukumu mbele ya macho ya walimwengu wakiukaji na wakandamizaji wa haki za binadamu.
-
Rais Rouhani: Marekani imeshindwa kwa fedheha katika njama ya kutaka kurefusha vikwazo vya silaha vya Iran
Aug 15, 2020 04:48Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezunguzia kufeli na kushindwa kihistoria Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusema: Marekani imeshindwa kwa fedheha na kidhalili katika njama zake za kutaka kurefusha muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.
-
Mousavi: Marekani haijawahi kutengwa kiasi hiki
Aug 15, 2020 02:11Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, haijawahi kushuhudiwa kuona Marekani ikitengwa kiasi hiki katika historia ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa. Sayyid Abbas Mousavi amebainisha hayo katika radiamali yake kwa kushindwa pakubwa Marekani mkabala na Iran katika Baraza la Usalama la UN.
-
Marekani yafedheheka baada ya mpango wake dhidi ya Iran kushindwa vibaya katika Baraza la Usalama
Aug 14, 2020 23:45Juhudi za Marekani za kutaka kuongezwa muhula wa vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimefeli na kugonga mwamba katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Spika wa Bunge la Iran: Imarati imejidhalilisha kwa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni
Aug 14, 2020 22:29Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa makubaliano ya Imarati na utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuanzisha uhusiano baina ya pande hizo mbili ni ya kijidhalilisha na ni usaliti kwa thamani za Umma wa Kiislamu na malengo ya taifa la Palestina.
-
Iran yapinga kimya cha wakala wa IAEA kuhusu shughuli za nyuklia za Saudia
Aug 14, 2020 22:29Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amepinga kimya cha Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kuhusu shughuli za siri za nyuklia za Saudi Arabia na silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Zarif: Wanaotumia vibaya mlipuko wa Beirut wanataka kuteteresha amani ya Lebanon
Aug 14, 2020 09:12Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran leo amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Waziri Mkuu wa Lebanon mjini Beirut na kusema kuwa, wanaotumia vibaya mlipuko mkubwa uliotokea katika bandari ya Beirut wana nia ya kuyumbisha amani ya Lebanon.
-
Iran: Uhusiano wa kidiplomasia wa Abu Dhabi na Tel Aviv ni ujinga wa kistratijia
Aug 14, 2020 03:37Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani hatua ya kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE au Imarati) na utawala wa Kizayuni wa Israel na kutaja hatua hiyo kuwa ni ujinga wa kistratijia ambao bila shaka utapelekea kuimarika mhimili wa muqawama na mapambano katika eneo.