Zarif: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono mapambano ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62839-zarif_jamhuri_ya_kiislamu_ya_iran_itaendelea_kuunga_mkono_mapambano_ya_wapalestina
Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumamosi usiku amefanya mazungumzo na Riyad al-Maliki Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono mapambano ya taifa la Palestina ili liweze kupata haki zake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 16, 2020 02:11 UTC
  • Zarif: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono mapambano ya Wapalestina

Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumamosi usiku amefanya mazungumzo na Riyad al-Maliki Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono mapambano ya taifa la Palestina ili liweze kupata haki zake.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Zarif ameongeza kuwa, kuna udharura hivi sasa kwa watu na makundi ya Palestina kuwa na umoja na mashikamano.

Kwa upande wake, Riyad Al Maliki ametoa shukrani zake za dhati kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na msimamo wake imara wa kuendelea kuunga mkono Palestina. Aidha amesema watu na viongozi wa Palestina wana azma imara ya kuendeleza mapambano hadi kufikia malengo yao ya kisheria. Aidha amesema: "Wapalestina wameungana na wako kitu kimoja katika kupigania ukombozi wa  ardhi za Palestina ambazo zinakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Siku ya Ijumaa pia Zarif alifanya mazungumzo ya simu na Ziad al-Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na pia Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).

Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alilaani vikali mapatano ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuanzisha uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia. Zarif amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima inaunga mkono malengo ya taifa la Palestina.

Riyad al-Maliki Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestin

Kufuatia hatua kadhaa zilizochukuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani kwa lengo la kurahisisha uanzishwaji uhusiano wa kawaida kati ya UAE na utawala haramu wa Kizayuni, Alkhamisi iliyopita pande hizo mbili za Abu Dhabi na Tel Aviv zilisaini mkataba na kuafikiana rasmi kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unatekeleza mkakati wa kuwa na uhusiano wa kawaida na tawala za Kiarabu huku ukiendeleza ukandamizaji wa Wapalestina sambamba na kukalia kwa mabavu maeneo ya Waarabu na maeneo matakatifu ya Kiislamu Palestina.