-
Araqchi akanusha madai ya kuwepo ofisi ya Taliban nchini Iran
Jul 19, 2020 10:06Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amekabidhisha vikali madai ya kipropaganda kuwa kundi la wapiganaji wa Taliban la Afghanistan lina ofisi hapa nchini. Sayyid Abbas Araqchi aidha amekanusha vikali uvumi wa uwepo wa kundi la Taliban hapa nchini Iran, kwa jina la "Baraza la Mashhad."
-
Ni bora Marekani ikiri imeshindwa na Iran badala ya kutoa vitisho vya kipuuzi
Jul 19, 2020 06:34Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametuma ujumbe kupitia Twitter akimhutubu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kwa kusema: "Itakuwa bora iwapo Washington itakiri kushindwa na Iran yenye nguvu badala ya kutoa vitisho vya kipuuzi na visivyoweza kutekelezeka."
-
Shamkhani amwambia Pompeo: Kukiri kushindwa na Iran ni bora kuliko bwabwaja za kijinga
Jul 18, 2020 22:21Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amejibu madai ya Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani na kusema kuwa, ni bora Washington ikiri kwamba, imeshindwa na Iran badala ya viongozi wake kuendelea na bwabwaja za kijinga.
-
Rais Rouhani: Iran inatengeneza aina tano za dawa za kutibu virusi vya corona
Jul 18, 2020 08:50Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kumefanyika kazi nzuri na muhimu sana hapa nchini kwa ajili ya kutengeneza dawa zenye taathira kubwa katika kutibu virusi vya corona na moja ya dawa hizo itaanza kutumiwa hapa nchini wiki kadhaa zijazo.
-
Hatua za Iran katika kutengeneza chanjo ya ugonjwa wa Covid-19
Jul 18, 2020 05:21Makundi mengi ya utafiti nchini Iran yanafanya kazi ya kuzalisha chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 maarufu kwa jina la corona; na hadi sasa mafanikio ya kutia moyo yamepatikana katika jitihada hizo za usiku na mchana.
-
Mkabataba Mkubwa wa ushirikiano wa Iran na China ni wa kukabiliana na ubeberu wa Marekani
Jul 18, 2020 03:35Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa zenye makao yao mjini Vienna Austria amesema kuwa, mkataba mkubwa wa ushirikiano baina ya Iran na China ni kwa ajili ya kukabiliana na ubeberu wa Marekani na fikra zake za kujikumbizia kila kitu upande wake.
-
Wanasayansi wa Iran wapiga hatua kubwa katika utengenezaji wa chanjo ya Corona
Jul 17, 2020 09:40Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran amesema timu kadhaa za wanasayansi nchini zimepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na kirusi cha corona.
-
Ushirikiano wa Russia na Iran ni kwa manufaa ya amani na usalama wa dunia
Jul 17, 2020 06:08Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia sambamba na kutangaza kuunga mkono suala la kulindwa na kudumishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na udharura wa kukabiliana na siasa za Marekani za uchukuaji maamuzi ya upande mmoja wamesisitiza juu ya kustawishwa zaidi uhusiano wa Tehran na Moscow.
-
Zarif: Iran haitalipa taifa lolote hata shibri moja ya ardhi yake
Jul 17, 2020 03:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria juu ya makubaliano ya miaka 25 ya ushirikiano kati ya Iran na China na kusisitiza kuwa, katu Jamhuri ya Kiislamu haitapeana hata shibri moja ya ardhi yake au kuipa nchi yoyote ile ikiwemo China, haki maalumu ya kutumia maeneo yake.
-
Brig. Jen. Shekarchi: Israel itashuhudia nguvu za Iran ikiendelea kufanya shari na uovu
Jul 16, 2020 22:48Msemaji wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa, iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaendelea kufanya shari na maovu yake, basi utakabiliwa na pigo kubwa kutoka kwa mrengo wa muqawama na Iran.