Hatua za Iran katika kutengeneza chanjo ya ugonjwa wa Covid-19
Makundi mengi ya utafiti nchini Iran yanafanya kazi ya kuzalisha chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 maarufu kwa jina la corona; na hadi sasa mafanikio ya kutia moyo yamepatikana katika jitihada hizo za usiku na mchana.
Akihojiwa jana Ijumaa kuhusu mafanikio hayo ya kiuatafiti, Daktari Saeed Namaki, Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran alieleza matarajio yake kuwa siku chache zijazo watawatangazia wananchi habari njema kuhusu jambo hilo.
Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran aidha ameashiria namna kundi la watafiti wa kisayansi 57 wanavyofanya kazi ya kutengeneza dawa ya kutibu ugonjwa wa Covid-19 na kuongeza kuwa, kundi hilo la wanasayansi wa Iran linafanya kazi kubwa ya kutafiti dawa na chanjo za maradhi hayo; ambapo matokeo ya utafiti wao yatachunguzwa katika kamati ya kielimu na inatazamiwa muda si mrefu chanjo iliyozalishwa na watafiti wa Kiirani itafanyiwa majaribio kwa binadamu. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya watu walioambukizwa kirusi cha corona duniani imepindukia milioni 14; huku watu karibu laki sita wakiwa wameaga dunia kwa maradhi hayo ya Covid-9. Wakati huo huo watu karibu 270,000 wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19 nchini Iran; na wengine karibu elfu 14 wameaga dunia.
Kiujumla kuna kadhia mbili kuu katika mchakato wa kukabiliana na ugonjwa huu hatari.
Kadhia ya kwanza: ni namna ya kukabiliana na kuenea kirusi cha corona ambapo kuna nafasi muhimu sana katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu. Wafanyakazi wa huduma za afya na matabibu wa Iran wamefanya kazi kubwa ya jihadi na kuweza kudhibiti kasi kubwa ya kuenea maambukizi ya corona licha ya kuanza wimbi la pili la maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19. Kiasi kwamba kuanzia jana Ijumaa mashirika ya ndege za nje yalirejea tena na kuanza kazi kama kawaida katika anga ya Iran kutokana na kuongezeka viashiria na hatua za udhibiti wa afya katika viwanja vya ndege.
Kadhia ya pili: ni juhudi za kurahisisha matibabu ya ugonjwa wa Covid-19. Hatua muhimu za Iran katika uwanja huo zinabainisha wazi kupiga hatua harakati za kisayansi na kitiba hapa nchini. Harakati hizo imeanza kwa kasi katika jamii ya kielimu ya nchi hii pamoja licha ya kuwepo matatizo mbalimbali yaliyosababishwa na kirusi cha corona.
Dakta Mostafa Ghanei, Mkuu wa Kamati ya Kielimu ya Kitengo cha Taifa cha Kupambana na Corona nchini Iran amesema: Ni nchi chache duniani mbazo wakati zinapokumbwa na wimbi kubwa la maambukizi ya virusi na likawa linahitajia suhula zote na vifaa vingi vya tiba vya kutambua wagonjwa wa ugonjwa huo ikaweza nchi hiyo katika muda wa miezi miwili tu; si tu kujitosheleza lakini pia ikaweza hata kuuza nje vifaa hivyo. Hii inaonyesha uwezo mkubwa wa kitekolojia wa Iran ikilinganishwa na nchi nyingine zilizodai kuwa na mfumo bora kabisa wa matibabu; na hii inatia moyo kwamba Iran inaweza kulindwa na wasomi na wanasayansi wazawa.
Sambamba na harakati hiyo; kazi nyingine muhimu za kielimu na kitafiti pia tayari zimeanza kwa ajili ya majaribio ya chanjo; kazi ambayo inapiga hatua vizuri sana. Matamshi ya Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran yanathibitisha nukta hiyo.
Watafiti wa Iran hivi sasa wanazifanyia majaribio chanjo na dawa bora za kutibu waathirika wa ugonjwa wa corona. Ni wazi kuwa matokeo ya utafiti huu wa Iran yanapaswa kutangaziwa nchi nyingine ili kuleta matumaini zaidi ya kudhibitiwa ugonjwa huo wa COVID-19.
Iwapo moja ya njia au dawa hizi zitakuwa na taathira; basi zitaingizwa katika protokali ya matibabu baada ya kuidhinishwa na Kamati ya Kielimu ya Kupambana na Corona ya humu nchini. Iran aidha inatambulika kuwa moja ya nchi zenye mchango na kufanya kazi kubwa katika katika utafiti wa kimataifa pia; kwani imeshiriki katika utafiti mwingi kimataifa. Michakato yote hiyo inaonyesha kuwa Iran kwa umakini inafanyia majaribio utafiti wa kielimu wenye itibari kuhusiana na corona. Watafiti nchini Iran wanatafuta njia mbalimbali za kutokomeza kirusi cha corona kwa kustafidi na mbinu za kisasa za kitiba na matibabu; na kama alivyobainisha Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu, Iran iko sambamba na nchi tano kubwa zinazofanya kazi ya kupata dawa na chanjo ya maradhi ya Covid-19 na haiko nyuma kabisa katika jitihada hizo.