-
Ushirikiano wa Russia na Iran ni kwa manufaa ya amani na usalama wa dunia
Jul 17, 2020 06:08Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia sambamba na kutangaza kuunga mkono suala la kulindwa na kudumishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na udharura wa kukabiliana na siasa za Marekani za uchukuaji maamuzi ya upande mmoja wamesisitiza juu ya kustawishwa zaidi uhusiano wa Tehran na Moscow.
-
Zarif: Iran haitalipa taifa lolote hata shibri moja ya ardhi yake
Jul 17, 2020 03:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria juu ya makubaliano ya miaka 25 ya ushirikiano kati ya Iran na China na kusisitiza kuwa, katu Jamhuri ya Kiislamu haitapeana hata shibri moja ya ardhi yake au kuipa nchi yoyote ile ikiwemo China, haki maalumu ya kutumia maeneo yake.
-
Brig. Jen. Shekarchi: Israel itashuhudia nguvu za Iran ikiendelea kufanya shari na uovu
Jul 16, 2020 22:48Msemaji wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa, iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaendelea kufanya shari na maovu yake, basi utakabiliwa na pigo kubwa kutoka kwa mrengo wa muqawama na Iran.
-
Rais Rouhani: Kuna wajibu kwa dunia kukabiliana na ubeberu wa Marekani
Jul 16, 2020 08:03Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na Rais Vladimir Putin wa Russia na mbali na kuishukuru Moscow kwa uungaji mkono wake kwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA, ameyahimiza mataifa ya dunia kusimama pamoja kukabiliana na ubeberu wa Marekani.
-
Takwimu za leo za ugonjwa wa corona Iran, zaidi ya wagonjwa laki mbili na 30 elfu wapata afueni
Jul 16, 2020 08:00Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, zaidi ya wagonjwa elfu mbili wa Covid-19 wamegunduliwa nchini katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, huku idadi ya waliopata afueni ya ugonjwa huo ikipindukia 230,000.
-
Safari ya Abbas Araqchi mjini Kabul; ushirikiano mzuri wa Iran na Afghanistan
Jul 16, 2020 07:49Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu anayehusika na masuala ya kisiasa amekutana na kufanya mazungumzo mjini Kabul na Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afganistan na kujadili masuala ya kupanua ushirikiano wa pande mbili katika nyanja zote
-
'Dawa ya kutibu virusi vya corona' iliyozalishwa hapa Iran kuingia sokoni karibuni
Jul 16, 2020 02:57Jamhuri ya Kiislamu ya Iran karibuni hivi itaanza kusambaza masokoni dawa ya kupambana na virusi ya 'Remdesivir' iliyozalishwa hapa nchini.
-
Wagonjwa zaidi ya 228,000 wa Covid-19 nchini Iran wamepata afueni
Jul 15, 2020 08:57Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, watu zaidi elfu mbili waliokumbwa na ugonjwa wa Covid-19 wamegunduliwa nchini, huku idadi ya waliopata afueni ya ugonjwa huo ikipindukia 228,000.
-
Rais Rouhani: Iran katu haitasalimu amri kwa mashinikizo ya madola makubwa hasa Marekani
Jul 15, 2020 08:28Rais Hassan Rouhani amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu katu haitasalimu amri kwa mashinikizo ya madola makubwa na hasa Marekani na akaongeza kwamba: Marekani ijue kwamba, kamwe haitafikia malengo yake licha ya hatua zake haribifu inazochukua dhidi ya maslahi ya taifa la Iran.
-
Zarif: Marekani inadhalilisha sheria na diplomasia na kuhatarisha usalama wa dunia
Jul 14, 2020 22:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametuma ujumbe kwa mnasaba wa mwaka wa tano wa kufikiwa mapatano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) na kusema: "Kitendo cha Marekani cha kudhalilisha sheria na udiplomasia ni jambo linalohatarisha usalama wa nchi hiyo na dunia kwa ujumla mbali na kuchafua jina la Washington katika uga wa kimataifa."