-
Zaidi ya watu laki moja na 66,000 wameshapata afueni baada ya kuugua COVID-19 nchini Iran
Jun 22, 2020 08:07Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran amesema kuwa, hadi hivi sasa zaidi ya watu laki moja na 66 elfu na 427 wameshapata afueni baada ya kuugua ugonjwa wa COVID-19 humu nchini na wameruhusiwa kurejea nyumbani.
-
Meli ya chakula ya Iran yafika kwenye eneo la majini la Venezuela licha ya vikwazo vya Marekani
Jun 22, 2020 03:17Meli ya Iran yenye chakula kwa ajili ya wananchi wa Venezuela imefika kwenye eneo la majini la nchi hiyo ya Amerika ya Latini licha ya Marekani kuiwekea vikwazo nchi hiyo na kuifungia njia zote. Hadi tunapokea habari hii, meli hiyo ilikuwa imekaribia kufika kwenye bandari ya Guaira.
-
Taarifa ya Bunge la Iran ya kulaani azimio la Bodi ya Magavana ya IAEA
Jun 22, 2020 02:43Wajumbe wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, jana Jumapili walitoa taarifa wakilaani azimio la Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) dhidi ya Iran na kusema azimio hilo ni mfano mwingine wa ubaguzi katika muundo wa wakala huo.
-
Salami: Uwezo mkubwa wa jeshi la Iran umewakosesha maadui hamu ya vita
Jun 21, 2020 23:28Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema utayarifu na uwezo mkubwa wa vikosi vya majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimewafanya maadui wa taifa hili wakose kuwa na hata ndoto ya kuingia katika makabiliano ya kijeshi na Iran.
-
Iran kuwa na jumla ya satalaiti 18 kufikia mwishoni mwa mwaka
Jun 21, 2020 23:21Kutokana na kuendelea kuboreka sekta ya anga za mbali ya Iran, Jamhuri ya Kiislamu inapania kuzalisha satalaiti zaidi na kufikisha jumla ya satalaiti 18 kufikia mwishoni mwaka huu wa Kiirani wa Hijria Shamsia, sawa na Machi 20, mwaka 2021.
-
Iran yakosoa kimya cha Ulaya mbele ya ukandamizaji na ukatili unaofanywa dhidi ya raia wa Marekani
Jun 21, 2020 06:27Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran kwa mara nyingine tena amekosoa kimya cha nchi za Ulaya mbele ya ukandamizaji na ukatili unaofanwa na vyombo vya dola vya serikali ya Marekani dhidi ya raia wa nchi hiyo.
-
Sisitizo la Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la kuimarishwa uwezo wa kiulinzi
Jun 21, 2020 04:27Maadui wa taifa la Iran wanapasa kutambua kuwa jina la kila shahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lina makumi ya makombora ambayo yanasubiri kukabiliana na kuharibu kabisa tishio lolote la karibu au mbali, kwa namna ambayo hata maadui wenyewe hawaifikirii.
-
Qalibaf: Wamagharibi kwa mara nyingine wamedhihirisha utambulisho wao hasimu
Jun 21, 2020 03:36Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, ametoa kauli baada ya Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kupitisha azimio dhidi ya Iran na kusema: "Nchi za Magharibi na hasa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kwa mara nyingine tena zimedhihirisha utambulisho wao hasimu na wa kutoaminika mbele ya taifa la Iran."
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: "Uhuru" hauna nafasi yoyote katika fikra za viongozi wa Marekani
Jun 20, 2020 23:14Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran imetangaza kuwa miaka mingi ya uporaji na vitisho imethibitisha kwamba "uhuru wa mtu mwingine" hauna nafasi yoyote katika fikra za maafisa wa serikali ya Marekani.
-
Rouhani: Iran imepata maksi nzuri katika kupambana na corona
Jun 20, 2020 07:29Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utendaji kazi wa Jamhuri ya Kiislamu katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19 umepata alama na maksi nzuri ikilinganishwa na nchi nyingine duniani hata zilizoendelea.