Rouhani: Iran imepata maksi nzuri katika kupambana na corona
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utendaji kazi wa Jamhuri ya Kiislamu katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19 umepata alama na maksi nzuri ikilinganishwa na nchi nyingine duniani hata zilizoendelea.
Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo Jumamosi katika kikao cha Kamati ya Taifa ya Kupambana na Ugonjwa wa COVID-19 na huku akisema kwamba ugonjwa wa corona umetoa pigo kali kwa nchi za dunia hasa katika sekta za mawasiliano na uchukuzi, utalii, uchumi, elimu na hata sekta ya michezo na kuongeza kuwa, kutokana na kambi ya kulinda usalama wa kiafya wa wananchi humu nchini kujitolea kikamilifu kwa kushirikiana na majeshi yote na wananchi wote, Iran imefanikiwa kupata maksi na alama nzuri katika vita dhidi ya corona.
Vile vile amesema, kulingaa na maelezo ya wanasayansi na wataalamu wa masuala ya tiba na matibabu, haiwezekani kutangaza ni lini hasa ugonjwa wa corona utaisha. Pia amesema, mtazamao wa wataalamu ni kwamba, kirusi cha corona hakiwezi kutoweka chenyewe hivyo tunapaswa kujiweka tayari kukabiliana nacho kwa muda mrefu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha amesisitiza kuwa, wataalamu wa afya na matibabu, serikali na wananchi wa Iran wameendelea kuwa kitu kimoja kama kawaida na kwamba kipindi hiki cha corona nacho kitapita kwa mafanikio ya taifa la Iran.
Hadi kufikia leo, idadi ya wagonjwa wa corona waliokuwa wameshapona nchini Iran walikuwa ni karibu laki moja na 61 elfu kati ya watu laki mbili na 2,584 waliothibitika kukumbwa na kirusi hicho humu nchini hadi leo mchana.