-
Iran: Utawala wa Kizayuni wa Israel umezaliwa kutoka katika tumbo la ugaidi
May 20, 2020 07:01Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa, utawala haramu wa Israel umezaliwa kutoka katika tumbo la ugaidi na umeendelea kupanda mbegu za vurugu na machafuko katika eneo hili la Asia Magharibi.
-
Onyo la viongozi wa Iran kwa Marekani kuhusu kusumbuliwa meli za mafuta za Iran
May 20, 2020 04:47Kutolewa ripoti kuhusu tishio la viongozi wa Marekani la kutaka kusumbua na kuzihangaisha meli za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinazoelekea Venezuela, kumewapelekea viongozi wa Iran watoe onyo kali dhidi ya hatua hiyo.
-
Meja Jenerali Bagheri: Minong'ono ya mwisho wa Israel ghasibu inasikika kwenye mitaa ya Tel Aviv
May 20, 2020 03:30Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Intifadha ya taifa la Palestina imeshavuka mipaka ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuingia kwenye awamu itakayoamua hatima yake na akasisitiza kwamba: Minong'ono ya kufikia tamati Israel ghasibu inasikika kwenye mitaa ya Tel Aviv.
-
Iran: Wamarekani wasimame kukabiliana na ubaguzi wa rangi wa kijamii
May 20, 2020 03:24Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitizia udharura wa wananchi wa Marekani kusimama imara kukabiliana na ubaguzi wa rangi wa kijamii ndani ya nchi hiyo.
-
Makamu wa Rais wa Iran: Vifaa vyote vinavyohitajika kukabiliana na corona vinazalishwa nchini
May 19, 2020 11:03Makamu wa Rais wa Iran wa Masuala ya Sayansi na Teknolojia amesema leo kuwa, mashirika ya elimu za utaalamu (knowledge-based) nchini yameunda vifaa vya kugundua virusi vya corona na akaongeza kuwa: Iran haihitaji kuagiza nje ya nchi vifaa inavyohitaji kwa ajili ya kukabiliana na corona kwa sababu mahitaji yote ya vifaa hivyo yanadhaminiwa humu humu nchini.
-
Dakta Kharrazi: Hatua za Upande mmoja za Marekani ni sumu angamizi kwa jamii ya kimataifa
May 19, 2020 02:24Mkuu wa Baraza la Kiistratijia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua za upande mmoja za Marekani ni sumu angamizi kwa jamii ya kimataifa na zinapelekea hali ya dunia izidi kuwa tata.
-
Kamati ya Bunge la Iran yaidhinisha muswada dhidi ya utawala wa Kizayuni
May 18, 2020 05:30Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiisalmu (Bunge la Iran) imeidhinisha muswada wa namna ambavyo Iran itakabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika upeo wa kitaifa na kimataifa.
-
Mousavi: Marekani inalenga kuvuruga mfumo wa nidhamu duniani
May 18, 2020 05:08Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Serikali ya sasa ya Marekani inalenga kusambaratisha nidhamu ya dunia sambamba na kuibua ghasia na nukta hii inapaswa kuwa kengele ya hatari kwa dunia.
-
Ayatullah Raisi: Kukombolewa Quds ni moja ya mambo yanayopewa kipaumbele na Umma wa Kiislamu
May 18, 2020 03:48Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua haribifu za Marekani na utawala haramu wa Israel katika eneo hili la Asia Magharibi na kusisitiza kuwa, kukombolewa Beitul-Muqaddas ni katika mambo yanayopewa kipaumbele na Umma wa Kiislamu.
-
Spika Larijani: Njama za utawala haramu wa Israel zinavuruga amani ya Asia Magharibi
May 18, 2020 03:48Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njama na hatua za chuki na uadui za utawala haramu wa Israel dhidi ya usalama na amani ya Asia Magharibi zinavuruga amani ya eneo hili.