Iran: Utawala wa Kizayuni wa Israel umezaliwa kutoka katika tumbo la ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61101-iran_utawala_wa_kizayuni_wa_israel_umezaliwa_kutoka_katika_tumbo_la_ugaidi
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa, utawala haramu wa Israel umezaliwa kutoka katika tumbo la ugaidi na umeendelea kupanda mbegu za vurugu na machafuko katika eneo hili la Asia Magharibi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 20, 2020 07:01 UTC
  • Iran: Utawala wa Kizayuni wa Israel umezaliwa kutoka katika tumbo la ugaidi

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa, utawala haramu wa Israel umezaliwa kutoka katika tumbo la ugaidi na umeendelea kupanda mbegu za vurugu na machafuko katika eneo hili la Asia Magharibi.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandikwa katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter wa wizara hiyo na kubainisha kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umezaliwa kutoka katika tumbo la ugaidi umefanya mauaji mengi dhidi ya wananchi wa Palestina na shakhsia mbali katika ulimwengu wa Kiarabu na hata maualama na wanazuoni wa Kiirani.

Taarifa hiyo imeeleza pia kuwa, katika kipindi cha miaka yote hii tangu kuasisiwa utawala bandia wa Israel utawala huo umeendelea kupanda mbegu za vurufu na machafuko katika eneo la Asia Magharibi.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza kuwa, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ni ukumbusho wa kila mwaka wa ulimwengu wa Kiislamu kwamba, utawala vamizi wa Israel na vitendo vyake vya kiuadui na kikatili vingali sababu kuu ya vurugu na machafuki katika eneo hili.

Aidha taarifa hiyo imebainisha kwamba, historia ya utawala ghasibu wa Israel imejaa uvamizi, hujuma, mauaji na mipango ya siri ya uundaji wa silaha za maangamizi ya umati, ukaliaji mabavu na uporaji wa ardhi na ukiukaji wa sheria.