Iran: Wamarekani wasimame kukabiliana na ubaguzi wa rangi wa kijamii
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61094-iran_wamarekani_wasimame_kukabiliana_na_ubaguzi_wa_rangi_wa_kijamii
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitizia udharura wa wananchi wa Marekani kusimama imara kukabiliana na ubaguzi wa rangi wa kijamii ndani ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 20, 2020 03:24 UTC
  • Iran: Wamarekani wasimame kukabiliana na ubaguzi wa rangi wa kijamii

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitizia udharura wa wananchi wa Marekani kusimama imara kukabiliana na ubaguzi wa rangi wa kijamii ndani ya nchi hiyo.

Katika ujumbe iliotuma kwenye akaunti yake ya Twitter kwa anuani ya: "Urithi wa Malcolm X inapasa udumishwe", Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeeleza kuwa: "Malcolm X alijitolea maisha yake kupigania uadilifu kwa ajili ya watu wanyonge walionyimwa fursa za kijamii; na sambamba na hilo aliendesha mapambano kwa muda mrefu kwa lengo la kufuta na kutokomeza hisia za Weupe kujiona bora zaidi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekumbusha katika ujumbe wake huo kuwa: Wakati umewadia kwa wananchi wa Marekani wa kila tabaka kusimama na kukabiliana na ubaguzi wa rangi wa kijamii pamoja na "mhamasishaji" wake mkuu.

Malcolm X

Malcolm X, alikuwa mwanaharakati wa Kiislamu wa Marekani na mtetezi wa haki za binadamu, ambaye anajulikana kama mmoja wa shakhsia wakubwa zaidi miongoni mwa Wamarekani weusi wenye asili ya Kiafrika katika historia aliyeacha athari kubwa.

Mpigania haki huyo za Wamarekani weusi aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 21, 1965 na watu waliodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la Taifa la Uislamu (Nation of Islam).../