Mousavi: Marekani inalenga kuvuruga mfumo wa nidhamu duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61057-mousavi_marekani_inalenga_kuvuruga_mfumo_wa_nidhamu_duniani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Serikali ya sasa ya Marekani inalenga kusambaratisha nidhamu ya dunia sambamba na kuibua ghasia na nukta hii inapaswa kuwa kengele ya hatari kwa dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 18, 2020 05:08 UTC
  • Mousavi: Marekani inalenga kuvuruga mfumo wa nidhamu duniani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Serikali ya sasa ya Marekani inalenga kusambaratisha nidhamu ya dunia sambamba na kuibua ghasia na nukta hii inapaswa kuwa kengele ya hatari kwa dunia.

Sayyid Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyasema hayo katika kikao na waandishi habari ambapo ameashiria baadhi ya hatua haribifu ambazo Rais Donald Trump wa Marekani amechukua na kusisitiza kuwa: "Serikali na mataifa ya dunia yanapaswa kutetea thamani za dunia na mafanikio ya kimataifa ambayo yamesisitizwa katika Hati ya Umoja wa Mataifa."

Mousavi amesema tishio la wakuu wa Marekani la kuzuia meli za mafuta za Iran ni jambo la aibu na kuongeza kuwa: "Iwapo Marekani inahisi haiipendi nchi fulani hiyo haipaswi kuwa sababu ya kuvuruga mabadilishano ya kisheria baina ya nchi au kuweka vikwazo."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Marekani itabeba dhima ya chochote kinachoweza kutokea iwapo itachukua hatua isiyo ya busara dhidi ya meli za Iran.

Ameongeza kuwa, iwapo Marekani itachukua hatua yoyote dhidi ya meli za Iran ambazo zinafanya kazi kisheria itakumbwa na radiamali kali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Mousavi aidha amesema Iran imefurahishwa na matukio ya kisiasa ya Iraq na Afghanistan. Kuhusiana na matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuhusu uwepo wa Iran nchini Syria, amesema: "Jamhuri ya Kiislamu imetuma washauri wake Syria kufuatia mwaliko wa serikali ya kisheria ya nchi hiyo, kwa ajili ya kukabiliana na ugaidi. Uwepo wa Iran nchini Syria hauna uhusiano wowote na Marekani na utawala wa Kizayuni."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds  ambayo yatafanyika Ijumaa ya mwisho  ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuongeza kuwa: "Maandamano ya Siku ya Quds yataendelea hadi mwisho wa utawala ghasibu na unaotenda jinai wa Kizayuni."