-
Barua ya klabu ya kutetea waathirika wa ugaidi kwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani; sisitizo la kufichuliwa ukweli wa tukio la Septemba 11
May 18, 2020 03:46"Kutosikilizwa sauti ya waliodhulumiwa, wanaotafuta ukweli ulio nyuma ya pazia la wapangaji wa tukio la Septemba 11, kutakuwa na taathira mbaya kwa tunu za haki za binadamu na usalama wa dunia; na kwa upande mwingine kunatoa baraka kamili kwa wapangaji na waandaaji sera walio nyuma ya pazia la ugaidi ili waendelee kutenda jinai na kupanga sera za ugaidi wakiwa na kinga kamili."
-
Kiongozi Muadhamu: Wamarekani hawataweza kubaki, si Iraq wala Syria na hakuna shaka watafukuzwa tu
May 17, 2020 23:15Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, kuwasha moto wa vita katika nchi kadhaa ikiwemo Afghanistan, Iraq na Syria ni miongoni mwa sababu za kuchukiwa Marekani na akabainisha kwamba, Wamarekani wanaeleza kinagaubaga kuwa 'tumeweka vikosi Syria kwa sababu kuna mafuta'; lakini bila shaka hawataweza kubaki, si Iraq wala Syria. Ni lazima waondoke huko na hakuna shaka kuwa wataondoshwa tu.
-
Waziri wa Afya: Iran sasa imebadilika kuwa msafirishaji na muuzaji wa bidhaa za utabibu
May 17, 2020 03:45Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran amesema, wakati mripuko wa virusi vya corona ulipozuka nchini kulikuwepo na uhaba fulani, lakini kwa kutegemea uwezo wake wa ndani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliweza ndani ya muda wa chini ya miezi miwili kubadilika kuwa msafirishaji na muuzaji badala ya kuagiza bidhaa za tiba kutoka nje.
-
Ombi la Umoja wa Mataifa kuhusu kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran
May 17, 2020 02:17Baada ya serikali ya Rais Donald Trump kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) mwaka 2018 katika fremu ya sera za mashinikizo ya juu kabisa na kisha kushadidisha vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa katika historia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na licha ya kuibuka ugonjwa wa COVID-19 nchini Iran, lakini bado Trump anasisitiza kuendeleza vikwazo vyake vilivyo dhidi ya ubinadamu dhidi ya taifa hili.
-
Corona; Utayari wa Iran wa kuzipatia nchi zingine tajiriba na uzoefu wake
May 16, 2020 21:56Richard Brennan, mkuu wa ujumbe wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uliotumwa mjini Tehran, miezi miwili nyuma wakati mripuko wa virusi vya corona ulipokuwa umeshavuka hata mipaka ya Iran alisema, Iran ni moja ya nchi zenye mifumo imara zaidi ya kiafya katika eneo la mashariki ya Mediterania na akasisitiza kuwa "kubadilishana taarifa kuna umuhimu mkubwa sana kwa dunia; na mafanikio iliyopata Iran katika suala la corona inapasa zipatiwe pia nchi zingine."
-
Rouhani: Iran itaadhimisha Siku ya Quds kwa kuzingatia kanuni za afya
May 16, 2020 21:55Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Siku ya Kimataifa ya Quds itaadhimishwa nchini Iran na pia Swala ya Idul FItr itaswaliwa kwa kuzingatia kanuni za afya kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19.
-
Waliopona ugonjwa wa COVID-19 nchini Iran wakaribia 92,000
May 15, 2020 08:02Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma na Upashaji Habari ya Wizara ya Afya ya Iran ametangaza kuwa, hadi hivi sasa waathiriwa zaidi ya 91,836 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata afueni na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Zarif: Wenye imani za kuingiza vitakasaji mwilini wanadai kuwa ni washiriki katika JCPOA
May 15, 2020 03:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, ushiriki wa Marekani katika azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umeshafikia tamati.
-
Rouhani: Jamii ya kimataifa inapaswa kukomesha jinai za Israel dhidi ya Wapalestina
May 14, 2020 19:59Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema jamii ya kimataifa ina wajibu wa kuchukua hatua za kivitendo za kukomesha jinai dhidi ya binadamu, ukandamizaji na dhulma wanazofanyiwa Wapalestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Corona; dhihirisho la tabia ya kigaidi ya Marekani dhidi ya taifa la Iran
May 14, 2020 19:54Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, licha ya kuwa siku zote Marekani inajulikana kuwa ni nchi ya kigaidi, lakini si kwa kiwango hiki cha hata kuzuia bidhaa za afya na tiba zikiwemo dawa kuwafikia watu wa Iran.