-
Iran: Hakuna mpango wa kufanya mazungumzo yoyote na Marekani
May 12, 2020 03:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, hakuna mpango wa kufanya mazungumzo yoyote na Marekani kwa sababu Washington haiwezi kuaminika kwa mazungumzo inayofanya.
-
Iran yakanusha madai ya Marekani kuwa inakwamisha kubadilishana wafungwa baina ya nchi mbili
May 11, 2020 22:56Sayyid Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran usiku wa kuamkia leo Jumanne amejibu madai yaliyotolewa na Marekani iliyodai kuwa Tehran inakwamisha ubadilishanaji wafungwa baina ya nchi mbili.
-
Waliopona COVID-19 nchini Iran wafika 87,000; 45 wafariki
May 11, 2020 10:56Wizara ya Afya, Matibabu na Mafunzo ya Tiba ya Iran imetangaza kuwa, miongoni mwa watu 109,000 walioambukizwa ugonjwa wa COVID-19 hadi leo, zaidi ya 87 elfu wa wamepata afueni na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Askari 19 wa Jeshi la Majini la Iran wafa shahidi katika ajali
May 11, 2020 10:46Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Majini la Iran imetangaza kuwa manowari ya kilojistiki inayojulikana kama 'Konarak' ilikumbwa na ajali Jumapili wakati ikiwa katika oparesheni za mazoezi katika eneo la pwani la Jask na Chabahar ambapo wanajeshi kadhaa waliokuwa katika manowari hiyo wamekufa shahidi.
-
Fahari ya kudumu ya Iran katika mapambano dhidi ya corona, kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu
May 11, 2020 04:54Akizungumza siku ya Jumapili asubuhi kwa njia ya mawasilioano ya video na Tume ya Taifa ya Mapambano dhidi ya Corona, ambayo ilijumuisha wanachama wa tume hiyo na waku wa mikoa 31 ya humu nchini, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesifu utendaji wa wananchi na viongozi wao katika uwanja huo kuhusu masuala tofauti ya kijamii, kiutamaduni, kiafya, kitiba, kielimu, kiutendaji na kihuduma na kusema, utendaji huo umekuwa wa kijihadi.
-
Mousavi: Ni utawala muasi tu wa Marekani ndio unaoona fakhari kukiuka sheria za kimataifa
May 11, 2020 03:41Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, ni utawala muasi tu ndio unaoweza kuona fakhari kukhalifu majukumu uliyonayo kimataifa na kukiuka sheria za kimataifa.
-
Madai ya kipuuzi ya Mike Pompeo kuhusu mafanikio Marekani baada ya kujitoa katika mapatano ya JCPOA
May 11, 2020 02:31Baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuyakosoa vikali mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA, Mei 8 mwaka 2018 alichukua uamuzi wa upande mmoja wa kuiondoa nchi yake katika makubaliano hayo.
-
Waziri Mkuu wa Iraq apongeza uungaji mkono wa Iran katika vita dhidi ya ISIS
May 10, 2020 19:53Waziri Mkuu mpya wa Iraq ameipongeza na kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa msaada na uungaji mkono wake katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS).
-
Kiongozi Muadhamu: Uwezo wa uendeshaji, falsafa ya kijamii na akhlaqi; maeneo matatu iliyofeli Magharibi katika corona
May 10, 2020 09:24Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, uwezo wa uendeshaji, falsafa ya kijamii na akhlaqi ni maeneo matatu ambayo Magharibi imefeli katika janga la corona.
-
Polisi ya Iran yakamata zaidi ya tani nne za madawa ya kulevya mkoani Sistan na Baluchistan
May 10, 2020 09:04Kamanda wa jeshi la Polisi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mkoani Sistan na Baluchistan amesema, jeshi hilo limefanikiwa kukamata zaidi ya tani nne za mihadarati katika mipaka ya kusini mashariki mwa nchi.