Askari 19 wa Jeshi la Majini la Iran wafa shahidi katika ajali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i60918-askari_19_wa_jeshi_la_majini_la_iran_wafa_shahidi_katika_ajali
Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Majini la Iran imetangaza kuwa manowari ya kilojistiki inayojulikana kama 'Konarak' ilikumbwa na ajali Jumapili wakati ikiwa katika oparesheni za mazoezi katika eneo la pwani la Jask na Chabahar ambapo wanajeshi kadhaa waliokuwa katika manowari hiyo wamekufa shahidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 11, 2020 10:46 UTC
  • Askari 19 wa Jeshi la Majini la Iran wafa shahidi katika ajali

Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Majini la Iran imetangaza kuwa manowari ya kilojistiki inayojulikana kama 'Konarak' ilikumbwa na ajali Jumapili wakati ikiwa katika oparesheni za mazoezi katika eneo la pwani la Jask na Chabahar ambapo wanajeshi kadhaa waliokuwa katika manowari hiyo wamekufa shahidi.

Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa maelezo kuhusu namna ajali hiyo ilivyotokea. Taarifa hiyo imesema: "Kufuatia ajali hiyo iliyotokea wakati wa mazoezi ya manoari kadhaa za Jeshi la Majini, timu za uokoaji zilifika katika eneo la tukio haraka na kuweza kuwachukua majeruhi na waliokufa shahidi." Taarifa hiyo imesema waliojeruhiwa walifikishwa katika vituo vya matibabu haraka.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanajeshi 19 wamekufa shahidi katika tukio hilo na wengine 15 wamejeruhiwa na kwamba hali yao ni nzuri.

Manoari za Iran zikiwa katika mazoezi

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, manowari ya Konarak iliyokumbwa na ajali hiyo imepelekwa katika eneo maalumu kwa ajili ya uchunguzi wa kiufundi.

Taarifa ya Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema wanamaji jasiri wanaendelea kuwa tayari kuilinda nchi huku wakiwa na moyo wa kujitolea kufa shahidi. Aidha taarifa hiyo imesema uchunguzi kamili na wa kitaalamu utafanyika kuhusu tukio hilo na hivyo hakuna haja ya kueneza uvumi.