Waziri wa ulinzi aliyetimuliwa Ukraine: Ufisadi mkubwa unazuia kuhitishwa vita
-
Mykhailo Fedorov
Waziri wa ulinzi aliyefukuzwa kazi wa Ukraine amekosoa kiwango cha ufisadi nchini humo, akisema kwamba ufisadi uliokita mizizi unazuia kukomeshwa vita na ujenzi mpya wa Ukraine.
Mykhailo Fedorov amesema kuwa: "Kwa muundo wa sasa wa serikali ya Ukraine, mchakato wa kufanya maamuzi, na kiwango kikubwa cha ufisadi, haiwezekani kukomesha vita kwa ufanisi na kuweka msingi wa ujenzi mpya wa nchi."
Waziri wa Ulinzi aliyefukuzwa kazi wa Ukraine pia amesema kwamba tatizo hilo haliishii kwa watu maalumu, akieleza kuwa mamia ya watu katika serikali ya Ukraine wanahusika katika mitandao ya ufisadi ambayo imekuwa ikipata pesa kutoka kwenye bajeti ya serikali kwa miaka mingi, jambo ambalo limepunguza kasi ya mchakato sahihi wa kufanya maamuzi.
Akizungumzia operesheni ya hivi karibuni ya kupambana na ufisadi nchini Ukraine, Mykhailo Fedorov amesema kwamba mtandao uliopangwa wa ufisadi pamoja na ushiriki wa wabunge kadhaa wa nchi hiyo na maafisa wa Ofisi ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, ulikuwa miongoni mwa walengwa wa operesheni hiyo.
Fedorov alifutwa kazi mwezi uliopita baada ya kukosana na mkuu wa vikosi vya jeshi la Ukraine.