Kamanda Qaani: Palestina ni fikra iliyo hai na isiyobadilika
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i140914-kamanda_qaani_palestina_ni_fikra_iliyo_hai_na_isiyobadilika
Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema: "Suala la kukomboa Palestina, kuanzia baharini hadi mtoni, (ardhi ya Palestina kuanzia Bahari ya Mediterania hadi Mto Jordan) liko hai zaidi na linawezekana kutimizwa sasa kuliko hapo awali."
(last modified 2026-08-24T06:11:42+00:00 )
Aug 24, 2026 06:08 UTC
  • Brigedia Jenerali Esmail Qaani
    Brigedia Jenerali Esmail Qaani

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema: "Suala la kukomboa Palestina, kuanzia baharini hadi mtoni, (ardhi ya Palestina kuanzia Bahari ya Mediterania hadi Mto Jordan) liko hai zaidi na linawezekana kutimizwa sasa kuliko hapo awali."

Brigedia Jenerali Esmail Qaani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema kwamba upanuzi wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi na uhalifu wa Wazayuni katika ardhi ya Palestina ni jaribio la kukwepa mgogoro na mzozo mkubwa wa kijeshi, kiusalama, kisiasa na kijamii katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, na Wazayuni hawawezi kuficha kushindwa kwao kimkakati tangu Oktoba 7 mwaka 2023.

Brigedia Jenerali Qaani amesisitiza kuwa: "Palestina ni fikra ililyo hai na isiyobadilika; fikra ambayo, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, itabakia hai hadi pale haki itakapopata ushindi."

Matamshi hayo yanakuja huku Israel ikiendeleza mpango haramu wa ujenzi wa vitongojii vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina unaojulikana kwa jina la E1 katika Ukingo wa Magharibi, mashariki mwa Quds Mashariki inayokaliwa.

Mnamo Agosti 21, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alionya kwamba mpango wa E1 ni 'tishio dhidi ya kuanzishwa taifa la Palestina linaloungana".

Awali, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alikuwa amewaambia wavamizi wa Kizayuni kwamba ikiwa hawataondoka kusini mwa Lebanon kwa miguu yao wenyewe, watafukuzwa kwa fedheha hali ya kuwa wameshindwa.

Brigedia Jenerali Esmail Qaani, aliandika kwenye ukurasa wake binafsi wa mitandao ya kijamii kwamba: "Wavamizi na magaidi wa Kizayuni! Msipoondoka kusini mwa Lebanon kwa miguu yenu wenyewe, tukio kuu la mwaka wa 2000 litakaririwa; mwaka uleule mliokimbia kusini mwa Lebanon kwa madhila."