-
Shehena muhimu zaidi ya satelaiti ya Iran ya Nahid-2 yafanyiwa majaribio
Sep 27, 2025 06:54Shehena kuu wa setilaiti ya Nahid-2 ya Iran, ambayo ilizinduliwa mwezi Agosti, kwa sasa inafanyiwa majaribio katika obiti. Shehena hiyo ina jukumu muhimu katika kuanzisha mawasiliano ya satelaiti.
-
Larijani: Utawala wa Kizayuni hauna huruma na nchi yoyote
Sep 27, 2025 06:53Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran ambaye amewasili Beirut kuhudhuria kikao cha Baraza la Kumbukumbu za Mashahidi wa Muqawama wa Hizbullah amesema kwamba, utawala wa Kizayuni hauna huruma na nchi yoyote ile.
-
Rais wa Iran: Sera za Trump zitateketeza eneo zima na Iran itatoa jibu kali kwa wavamizi
Sep 27, 2025 03:14Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema sera za rais wa Marekani ziko kwenye mkondo wa kuibua mabadiliko makubwa na vurugu katika eneo lote la Asia ya Magharibi, akionya kuwa Iran itakabiliana na wavamizi wowote kwa nguvu ya juu kabisa iwapo kutatokea uvamizi mpya wa kijeshi.
-
Iran na Russia zasaini mkataba wa dola bilioni 25 kuhusu ujenzi wa mitambo ya nyuklia
Sep 27, 2025 03:11Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia zimesaini mkataba wa dola bilioni 25 kwa ajili ya kujenga mitambo minne ya nishati ya nyuklia, kama sehemu ya makubaliano ya muda mrefu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tehran na Moscow katika nyanja mbalimbali.
-
Iran: Kura ya 'snapback' ni batili, haina mashiko ya kisheria
Sep 26, 2025 23:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesisitiza kuwa, juhudi za mataifa matatu ya Ulaya ya Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani za kuhuisha vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kwa kutumia utaratibu unaojulikana kama snapback' ni "batili na hazina mashiko yoyote ya kisheria."
-
Pezeshkian: Iran iko ‘tayari kabisa’ kwa hali yoyote iwapo mpango wa snapback utatekelezwa
Sep 26, 2025 07:28Rais Masoud Pezeshkian amesema kuwa Iran iko tayari kikamilifu kwa hali yoyote endapo nchi za Ulaya zitaendelea na hatua ya kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa kupitia kile kinachoitwa utaratibu wa snapback, na ameonya kwamba mazungumzo ya kidiplomasia yatakuwa hayana maana chini ya vikwazo vilivyorejeshwa.
-
Iran yaandaa moja ya maonyesho makubwa ya teknolojia za elektroniki, kompyuta na biashara ya mtandaoni
Sep 26, 2025 07:23Jiji la Tehran wiki hii ni mwenyeji wa ELECOMP 2025, maonyesho makubwa na yenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Iran yanayohusu teknolojia za elektroniki, kompyuta, na biashara kwa njia ya mtandao (e-commerce).
-
Marekani na washirika wake zaendelea kuiga kutengeneza droni maarufu ya Iran
Sep 26, 2025 03:00Nchi kadhaa duniani zikiongozwa na Marekani zinapigana vikumbo katika kuiga na kutengeneza nakala za ndege isiyo na rubani ya Shahed ya Iran, ambayo si ghali lakini yenye ufanisi na usahihi wa hali ya juu.
-
Rais Pezeshkian: Mazungumzo hayana maana ikiwa vikwazo vitarejeshwa
Sep 25, 2025 23:01Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa mazungumzo ya kidiplomasia hayatakuwa na maana iwapo kundi la nchi tatu za Ulaya E3 linaloundwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zitarejesha tena vikwazo dhidi ya Tehran.
-
Baghaei: Madai ya Marekani ya kuheshimu diplomasia ni chapwa na udanganyifu
Sep 25, 2025 08:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema katika kujibu madai ya Marekani ya kwamba eti iko tayari kufanya mazungumzo na Iran na kuheshimu diplomasia na kusema: Huwezi kupiga nchi kwa mabomu na baadaye kudai eti unaheshimu mazungumzo ya kidiplomasia.