Iran yawakamata vinara 300 wa ghasia zilizochochewa kutoka nje ya nchi
Wizara ya Usalama ya Iran imesema kuwa zaidi ya watu 300 ambao ni vinara wakuu na waratibu wa ghasia za hivi karibun nchini, ghasia ambazo zimechochewa na madola ya kigeni, wamekamatwa.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, ukamataji huo ulifanyika kufuatia taarifa na utambuzi uliotolewa na wananchi waliowabaini waliokuwa wakihusika na vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibifu mnamo Januari 8.
Wizara ilisema kuwa kwa msaada wa wananchi, vikosi vya usalama vimeweza kuwafuatilia na kuwakamata zaidi ya watu 300 wanaohusishwa moja kwa moja na matendo hayo ya uhalifu.
Aidha, wizara iliongeza kuwa baadhi ya taarifa zilizotolewa na umma zimechangia pia kukamatwa kwa makundi yenye silaha ya kigaidi, ambayo yalikuwa na nia ya kuwadhuru raia au kuwashambulia maafisa wa usalama wakati wa machafuko hayo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ushirikiano wa wananchi katika kutoa taarifa juu ya vitisho hivyo umeongeza ari na morali ya vikosi vya usalama.
Ingawa maafisa wengi wa usalama walijeruhiwa katika vurugu hizo, wizara imesema wanaendelea kutekeleza majukumu yao bila kusita.
Wizara pia imewahimiza wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za kiusalama kwa kutoa taarifa zozote kuhusu watu wenye silaha au washiriki wa ghasia za hivi karibuni.
Kile kilichoanza mwishoni mwa mwezi uliopita kama maandamano ya amani dhidi ya hali ngumu ya kiuchumi nchini Iran, kiligeuka kuwa vurugu baada ya matamko ya hadharani kutoka kwa maafisa wa Marekani na utawala wa Israel ambay yalichochea uharibifu na machafuko.
Wakati wa machafuko hayo, mamlaka zinasema kuwa mamluki wanaoungwa mkono na madola ya kigeni walivamia miji mbalimbali, wakaua maafisa wa usalama na raia, na kusababisha uharibifu wa mali za umma.
Rais wa Marekani ametishia mara kadhaa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran akidai kuwa anaunga mkono wafanya ghasia wenye silaha.