Uzalishaji na mauzo ya nje ya chuma Iran yaongezeka kwa asilimia 27
Iran imeripoti ongezeko kubwa la mauzo yake ya nje ya chuma na chuma ghafi katika kipindi cha miezi tisa kilichomalizika mwishoni mwa Desemba, hatua inayoendana na juhudi za nchi hiyo kupanua vyanzo vyake vya mapato nje ya mafuta.
Kwa mujibu wa ripoti ya Jumapili ya shirika la habari la Tasnim, ikinukuu takwimu za Chama cha Wazalishaji wa Chuma cha Iran (ISPA), mapato ya mauzo ya nje ya chuma na chuma ghafi yalifikia dola bilioni 6.048 kati ya Aprili na Desemba ikiwa ni ongezeko la asilimia 27 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2024.
Kwa upande wa kiasi, usafirishaji wa chuma nje ya nchi uliongezeka kwa asilimia 43 na kufikia tani milioni 30.393, kwa mujibu wa takwimu hizo.
Mauzo ya nje ya bidhaa za chuma zilizokamilika yalifikia tani milioni 3.331 zenye thamani ya dola bilioni 1.542 ikiwa ni ongezeko la asilimia 19 kwa kiasi na asilimia 10 kwa thamani ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.
Mauzo ya nje ya mild steel (chuma cha nusu-kukamilika) yalipanda kwa asilimia 39 kwa kiasi na kufikia tani milioni 6.136, yakizalisha mapato ya dola bilioni 2.528—ongezeko la asilimia 24 mwaka hadi mwaka.
Chuma cha nusu-kukamilika huwa na aina tatu za ingots za chuma ambazo ni billet, bloom, na slab, ambazo hutumika kutengeneza bidhaa za chuma zilizokamilika.
Iran imeona ongezeko kubwa katika uzalishaji na mauzo yake ya nje ya chuma tangu nchi hiyo iwekwe chini ya vikwazo vya Marekani mwaka 2018.
Mwelekeo huo mpya umeisaidia Iran kupanua uchumi wake na kupunguza utegemezi wa mapato yatokanayo na mauzo ya mafuta ghafi ya petroli.
Takwimu za ISPA zinaonyesha kuwa mauzo ya nje ya chuma ghafi pia yalipanda kwa kasi katika kipindi cha miezi tisa hadi mwishoni mwa Desemba, yakipata dola bilioni 1.977 ikiwa ni ongezeko la karibu asilimia 50 na kiasi kiliongezeka kwa zaidi ya asilimia 49 hadi tani milioni 20.927.
Kwa upande wa uzalishaji, bidhaa za chuma zilizokamilika ziliongezeka kwa asilimia 1 na kufikia tani milioni 16.647; uzalishaji wa chuma cha katiulipanda kwa asilimia 7.4 hadi tani milioni 24.708; na uzalishaji wa chuma ghafi uliongezeka kwa asilimia 6.72 hadi tani milioni 140.2 katika kipindi cha Aprili–Desemba mwaka hadi mwaka.