-
Kamanda Hajizadeh: Leo hii Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni dola kubwa
Apr 24, 2020 02:39Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, leo hii, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni dola kubwa na kwamba Marekani haiwezi kulifanyia upuuzi wowote taifa kubwa la Iran.
-
Iran: Tuko tayari kuwasaidia wananchi wa Marekani wanaoteseka kwa corona
Apr 24, 2020 02:39Waziri wa Afya wa Iran amejibu maneno ya kijuba ya waziri wa afya wa Marekani aliyedai kuwa nchi yake iko tayari kuisaidia Iran kupambana na corona akisisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonesha kivitendo uwezo wake mkubwa wa kakabiliana na matatizo kama haya ya corona na kuongeza kuwa, Tehran iko tayari kuwasaidia wananchi wa Marekani wanaoteseka kwa maradhi ya COVID-19 hivi sasa kutokana na uzembe wa serikali yao.
-
Iran yalaani chokochoko za Marekani Ghuba ya Uajemi, yamuita balozi wa Uswisi
Apr 23, 2020 22:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali chokochoko za jeshi la Marekani dhidi ya wanajeshi wa baharini wa Iran katika Ghuba ya Uajemi, sambamba na kukosoa bwabwaja na vitisho vya Rais Donald Trump dhidi ya askari hao wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH).
-
Iran yajibu bwabwaja mpya za Trump; yasema: Tutajibu vikali uchokozi wowote Ghuba ya Uajemi
Apr 23, 2020 07:14Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, usalama na amani katika eneo la Ghuba ya Uajemi ni katika masuala muhimu mno kwa Iran kwani usalama wa eneo hilo ni jambo la kiistratijia kwa Tehran hivyo chokochoko na vitisho vyovyote kwenye eneo hilo vitajibiwa vikali na kwa haraka sana.
-
Karibu asilimia 65 ya waathiriwa wa corona wapata uzima nchini Iran
Apr 23, 2020 07:06Wizara ya Afya, Matibabu na Mafunzo ya Tiba ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa waathiriwa 64 elfu na 843 wa ugonjwa wa corona humu nchini wamepata uzima na wameruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Utawala bandia wa Kizayuni wapatwa na hasira kali kufuatia kurushwa angani kwa mafanikio satalaiti ya Iran
Apr 23, 2020 03:49Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala Haramu wa Israel imetoa taarifa ya kulaani kurushwa angani kwa mafanikio, satalaiti ya Iran inayojulikana kama Nour-1.
-
Brigedia Jenerali Amir Hatami: Jeshi la Iran limejiweka tayari kukabiliana na vitisho vyovyote vile
Apr 23, 2020 03:10Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uadui wa kijeshi wa madola ya kibeberu na yenye fitina dhidi ya nchi hii kwa kipindi cha miongo minne iliyopita na kusema kuwa, jeshi la Iran limejiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vyovyote vile.
-
Marais Rouhani na Museveni wataka kuimarishwa uhusiano wa Iran na Uganda
Apr 22, 2020 08:38Rais Hassan Rouhani ameutaja uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uganda kuwa mzuri na uliojengeka katika misingi ya heshima, na kusisitiza kuwa Iran iko tayari kuboresha uhusiano wa pande mbili na nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika nyuga zote.
-
Iran ina uwezo wa kutuma kifaa cha kupima Corona nje ya nchi
Apr 22, 2020 08:25Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili lina uwezo wa kutuma nje ya nchi kifaa cha kupima virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19.
-
Jeshi la IRGC larusha satalaiti ya kwanza ya kijeshi ya Iran katika anga za mbali + Video
Apr 22, 2020 03:40Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limerusha kwa mafanikio satalaiti ya kwanza ya kijeshi ya Iran katika anga za mbali.