-
Ripoti: Idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa katika vita dhidi ya Iran yazidi takwimu rasmi za Idara ya Vita
Sep 20, 2026 04:31Inawezekana kuwa idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa katika maeneo mbalimbali ya Asia Magharibi wakati wa vita dhidi ya Iran vilivyoendeshwa na utawala wa Trump ni kubwa kuliko inavyoonyeshwa katika “rekodi za waathirika” zinazopatikana hadharani kutoka Idara ya Vita ya Marekani.
-
Qalibaf asema enzi ya ndege za Marekani aina ya F-35 “kuwindwa” imeanza
Sep 19, 2026 11:59Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema enzi ambayo ndege za kisasa kabisa za kivita za Marekani aina ya F-35 na F-15 zinafuatiliwa na kulengwa tayari imeanza, wakati ripoti zikionyesha kuongezeka kwa shinikizo na uharibifu kwa jeshi la Marekani, miezi saba baada ya Washington kuanzisha vita haramu dhidi ya Iran.
-
“Machozi ya kinafiki”: Araghchi amjibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa kuhusu madai ya haki za binadamu
Sep 19, 2026 11:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amejibu madai ya hivi karibuni yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noël Barrot, aliyeshutumu Iran kwa ukiukaji wa haki za binadamu, huku akiikosoa Paris kwa ukimya wake kuhusu mauaji ya watoto wa shule wa Iran yaliyosababishwa na Marekani.
-
Iran yamnyonga jasusi wa utawala wa Israel aliyetoa taarifa za maeneo ya kijeshi
Sep 19, 2026 11:51Idara ya Mahakama ya Iran imetangaza kutekelezwa kwa hukumu ya kifo kwa kunyongwa Hossein Pedaran, ambaye alitiwa hatiani kwa makosa ya ujasusi na kutoa taarifa nyeti kuhusu vituo vya kijeshi vya Isfahan kwa shirika la kijasusi la utawala wa Kizayuni, Mossad.
-
Je, madhara ya uchokozi wa kijeshi dhidi ya Iran yameathiri vipi uchaguzi wa Marekani?
Sep 19, 2026 07:43Uchokozi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya Iran umefikia hatua ambapo athari zake zinavuka mipaka ya moja kwa moja ya eneo la mgogoro.
-
Maafisa 6 wa Marekani: Idadi ya Wamarekani waliouawa katika vita na Iran ni zaidi ya takwimu za Pentagon
Sep 19, 2026 03:09Wakati Wizara ya Vita ya Marekani ikidai kuwa wanajeshi 18 wameuawa hadi sasa katika vita na Iran, maafisa sita waandamizi wa Marekani wamekanusha madai hayo na kusema kuwa, idadi ni kubwa zaidi na inayotolewa na vyombo rasmi.
-
Al-Hajj Ali-Akbari: Hatutofanya mazungumzo hadi masharti ya Kiongozi Muadhamu yatimizwe
Sep 18, 2026 11:02Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema kuwa: "Hakutakuwa na mazungumzo yoyote hadi pale masharti yote yaliyowekwa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu yatakapotimizwa. Kwa taufiki ya Allah, tutaendelea kuwa macho mbele ya njama hatari za adui."
-
Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa: Marekani imetenda uhalifu wa kivita nchini Iran
Sep 18, 2026 03:54Tume ya Kutafuta Ukweli ya Umoja wa Mataifa imetangaza kwamba, baada ya kufanya uchunguzi na kuchambua ushahidi, imefikia hitimisho kwamba mashambulizi ya Marekani dhidi ya Minab na Lamerd yalikuwa ni uhalifu wa kivita.
-
Baghaei ajibu madai ya Saudi Arabia kuhusu kushambuliwa mji mtakatifu wa Makka
Sep 18, 2026 03:52Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, madai ya kuzuia ndege isiyo na rubani iliyokuwa ikielekea katika mji mtakatifu wa Makka hayawezi kuwa msingi wa kuutuhumu upande wowote.
-
Iran yajibu mapigo, yamtimua mwanadiplomasia wa Sweden
Sep 18, 2026 03:50Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, sanjari na kukanusha madai ya Sweden dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, imempa mwanadiplomasia wa nchi hiyo aliyeko Tehran muda wa saa 48 kuondoka nchini, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi kwa uamuzi wa Stockholm wa kukataa kumruhusu mwanadiplomasia wa Iran kuendelea na shughuli zake.