Ayatullah Khamenei awapongeza Wairaqi kwa mahudhurio makubwa katika mazishi ya Kiongozi shahidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139998-ayatullah_khamenei_awapongeza_wairaqi_kwa_mahudhurio_makubwa_katika_mazishi_ya_kiongozi_shahidi
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei amewashukuru watu wa Iraq kwa mapokezi "makubwa" na mahudhurio yao ya kustaajabisha katika mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, akisema tukio hilo linaonyesha uhusiano mkubwa wa kidini na kihistoria kati ya mataifa ya Iran na Iraq.
(last modified 2026-07-19T12:01:39+00:00 )
Jul 19, 2026 09:29 UTC
  • Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
    Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei amewashukuru watu wa Iraq kwa mapokezi "makubwa" na mahudhurio yao ya kustaajabisha katika mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, akisema tukio hilo linaonyesha uhusiano mkubwa wa kidini na kihistoria kati ya mataifa ya Iran na Iraq.

Katika ujumbe aliotumwa kwa mamlaka kuu za kidini, wasomi, viongozi wa makabila, wanafikra na watu wa Iraq jana Jumamosi, Ayatullah Khamenei amewapongeza Wairaqi kwa kuandaa "hamasa adhimu na yenye maana kubwa" iliyoambatana na hisia za huzuni, kujitolea na uaminifu.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amehusisha ushiriki mkubwa wa taifa hilo la Kiarabu katika tukio hilo na urithi wa kidini wa muda mrefu wa nchi hiyo na historia yake ya kuunga mkono Kambi ya Muqawama (Resistance Front) ya kikanda - ambayo iliimarishwa kwa nguvu katika mapambano yake dhidi ya ubeberu wa kimataifa na utawala wa Kizayuni chini ya Kiongozi aliyeuawa shahidi.

Akizungumzia shughuli hiyo ya mazishi, Ayatullah Khamenei amesema Wairaqi walimkaribisha Kiongozi aliyeuawa shahidi "kwa mioyo yao yote" wakati mwili wake ulipohamishiwa kwenye haramu takatifu katika miji ya Najaf na Karbala kwa ajili ya mazishi, akitaja shughuli hiyo kuwa ni onyesho lisilo na mfano la mshikamano kati ya watu wa Iran na Iraq.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema idadi kubwa ya watu waliojitokeza katika shughuli hiyo ilionyesha kushindwa njama za watawala wa nchi za kibeberu duniani za kutaka kuibua mgawanyiko kati ya mataifa hayo mawili jirani.

"Ushiriki wa makumi ya mamilioni ya watu nchini Iran na Iraq uliashiria mwanzo wa ukurasa mpya ya mwamko na ushiriki hai unaolenga kupindua milinganyo iliyopangwa awali na mataifa ya kibeberu," ujumbe huo umesema.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa Marekani imetambua kwamba dhana ya kuendeleza "uwepo wake usiopingwa na yeyete" katika eneo la Magharibi mwa Asia "si chochote zaidi ya njozi butu isiyo na maana."

Ujumbe huo umefuatia shughuli ya mazishi ya marehemu Ayatullah Ali Khamenei nchini Iraq ambapo serikali ya Iraq ilisema ilishirikisha waombolezaji zaidi ya milioni 10 katika miji ya Najaf na Karbala, na kufanya tukio hilo kuwa mojawapo ya mkusanyiko mkubwa zaidi wa mazishi katika historia ya kisasa ya miji hiyo miwili.