-
Ujumbe wa mwaka mpya wa Kiongozi Muadhamu; kuvuka matatizo na mustakbali wenye matumaini
Mar 20, 2020 04:55Katika ujumbe wake alioutoa asubuhi ya leo Ijumaa kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya wa Kiirani wa 1399, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria kusadifiana kwa siku ya kwanza ya mwaka huu na kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Musa bin Jaffar (as), ambapo ametoa mkano wa pole na maombolezo kwa mnasaba huo na kisha kulitakia heri na fanaka taifa la Iran na hasa familia za mashahidi na wanajihadi wa medani ya afya na tiba, kwa mnasaba wa mwaka huu mpya.
-
Kiongozi Muadhamu: Mwaka mpya wa 1399 ni Mwaka wa Ustawi Mkubwa katika Uzalishaji
Mar 20, 2020 04:54Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka mpya wa 1399 Hijria Shamsia ulioanza leo nchini Iran kuwa ni Mwaka wa Ustawi Mkubwa katika Uzalishaji na kusema: Hatua kubwa ya uzalishaji inapaswa kuleta mabadiliko yanayohisika katika maisha ya wananchi.
-
Rais Rouhani: Mwaka uliopita ulijaa hamasa kubwa ya wananchi wa Iran
Mar 20, 2020 04:53Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika ujumbe wake wa mwaka mpya wa 1399 Hijria Shamsia kwamba: Mwaka uliopita ulikuwa mwaka wa matukio na hamasa nyingi, na kwamba matukio makubwa zaidi katika historia ya nchi hii na hamasa zenye fahari kubwa zimetengenezwa na wananchi mashujaa wa Iran katika mwaka huo.
-
Karibu watu 6000 walioathirika na virusi vya Corona wamepona nchini Iran
Mar 19, 2020 23:10Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Kidaktari nchini Iran imetangaza kwamba, hadi sasa watu 5,979 walioathirika na virusi vya Corona hapa nchini, wamepona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
-
Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na miito inayoongezeka ya kuondolewa vikwazo hivyo
Mar 19, 2020 10:03Licha ya kuibuka virusi angamizi vya Corona ulimwenguni ikiwemo Iran na kuweko ulazima wa walimwengu wote kukabiliana navyo, lakini Marekani ingali inang’ang’ania kuendeleza utendaji wake wa kivikwazo katika fremu ya sera za vikwazo vya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran na imekuwa ikitangaza mtawalia vikwazo vipya dhidi ya Tehran.
-
Iran ni nchi pekee duniani ambayo hairuhusiwi kununua dawa kimataifa
Mar 19, 2020 09:09Balozi wa Iran nchini Uhispania Hassan Qashqavi amekosoa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema, vikwazo hivyo vimeizuia Iran kununua dawa na vifaa vya tiba katika soko la kimataifa.
-
Mzee mwenye umri wa miaka 90 aboreka afya baada ya kuambukizwa corona Iran
Mar 19, 2020 08:55Mzee mwenye umri wa miaka 90 ambaye alikuwa ameambukizwa ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona nchini Iran ameboreka afya na kuruhusiwa kuenda nyumbani baada ya kulazwa hospitalini.
-
Iran yazikosoa nchi za Kiarabu kwa kuzuia taarifa ya NAM ya kulaani vikwazo vya US
Mar 19, 2020 04:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali hatua ya baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM, kwa kuzuia kutolewa taarifa ya jumuiya hiyo ya kulaani vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran.
-
Bikizee wa miaka 103 apona corona nchini Iran
Mar 18, 2020 09:39Ajuza na bikizee wa miaka 103 aliyekuwa ameambukizwa kirusi cha corona amepona nchini Iran na ameruhusiwa kurudi nyumbani kutoka hospitalini.
-
Shamkhani: Marekani ndiye mtuhumiwa wa kueneza corona, iache kupayuka, itoe majibu kwa walimwengu
Mar 18, 2020 09:36Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, upayukaji ndiyo mbinu maarufu inayotumiwa na Marekani ya kukwepa kujibu tuhuma zinazoikabili.