Rais Rouhani: Mwaka uliopita ulijaa hamasa kubwa ya wananchi wa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i59856-rais_rouhani_mwaka_uliopita_ulijaa_hamasa_kubwa_ya_wananchi_wa_iran
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika ujumbe wake wa mwaka mpya wa 1399 Hijria Shamsia kwamba: Mwaka uliopita ulikuwa mwaka wa matukio na hamasa nyingi, na kwamba matukio makubwa zaidi katika historia ya nchi hii na hamasa zenye fahari kubwa zimetengenezwa na wananchi mashujaa wa Iran katika mwaka huo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 20, 2020 04:53 UTC
  • Rais Hassan Rouhani
    Rais Hassan Rouhani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika ujumbe wake wa mwaka mpya wa 1399 Hijria Shamsia kwamba: Mwaka uliopita ulikuwa mwaka wa matukio na hamasa nyingi, na kwamba matukio makubwa zaidi katika historia ya nchi hii na hamasa zenye fahari kubwa zimetengenezwa na wananchi mashujaa wa Iran katika mwaka huo.

Katika ujumbe wake wa Nowruz, Rais Rouhani amezungumzia vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema kuwa: Maadui wa Iran wametekeleza vikwazo shadidi zaidi wakidhani kwamba, wananchi watasalimu amri lakini taifa kubwa la Iran limesimama kidete mbele ya mashaka hayo na kutengeneza hamasa ya idara madhuburi ya uchumi usiotegemea mafuta ambayo imetimia kwa mara ya kwanza hapa nchini katika miongo kadhaa ya hivi kariibuni. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ameongeza kuwa, Wamarekani walitaka kuitumbukiza Iran katika hali ya mgogoro kwa kuzidisha mfumuko wa bei na mgogoro wa uchumi, lakini kinyume chake, takwimu zote zinaonyesha kuwa, uchumi wa Iran ulikuwa na kuimarika katika miezi 9 ya  mwaka uliopita, na mfumuko wa bei umedhibitiwa kwa kiwango kikubwa. 

Rais Rouhani amesema: Hii leo katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa 1399 Hijria Shamsia akiba ya kistratijia ya Iran iko katika hali bora zaidi kuliko miaka iliyopita.

Ameongeza kuwa: Iran haijashindwa, imesimama kidete mbele ya mashinikizo ya Marekani na imeishinda Washington katika Mahakama ya Kimataifa, na kuinuka kifua mbele na kushinda katika duru zote za kimataifa na fikra za walimwengu katika upande wa masuala ya kisiasa.