Iran ni nchi pekee duniani ambayo hairuhusiwi kununua dawa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i59843-iran_ni_nchi_pekee_duniani_ambayo_hairuhusiwi_kununua_dawa_kimataifa
Balozi wa Iran nchini Uhispania Hassan Qashqavi amekosoa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema, vikwazo hivyo vimeizuia Iran kununua dawa na vifaa vya tiba katika soko la kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 19, 2020 09:09 UTC
  • Iran ni nchi pekee duniani ambayo hairuhusiwi kununua dawa kimataifa

Balozi wa Iran nchini Uhispania Hassan Qashqavi amekosoa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema, vikwazo hivyo vimeizuia Iran kununua dawa na vifaa vya tiba katika soko la kimataifa.

Katika mahojiano na gazeti la  Larasson la Uhispania, Qashqavi amesema Iran ni nchi pekee duniani ambayo inazuiwa kununua dawa katika soko la kimataifa na kuongeza kuwa, Marekani inazuia mashirika ya kimataifa kuiuzia Iran dawa na vifaa ya tiba. Ameongeza kuwa, Marekani inazizuia pia benki za kimataifa kushirikiana na Iran katika kununua vifaa muhimu vya tiba na dawa.

Balozi Qashqavi amesisitiza kuwa, vikwazo hivyo vya Marekani dhidi ya Iran ni 'dhulma ya wazi' ambayo inakiuka misingi yote ya ubinadamu.

Balozi wa Iran nchini Uhispania amesema ugonjwa wa COVID-19 au corona sasa ni chombo kinachotumiwa na Marekani kuzidisha mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Iran.

Aidha amesema Marekani inatumia vyombo vyake vya habari, ikiwa ni pamoja na kanali za televisehni za lugha ya Kifarsi kusambaza habari feki na ripoti zisizo na msingi lengo likiwa ni kupotosha fikra za umma kuhusu hatua zilizo dhidi ya ubinadamu zinazochukuliwa na Washington.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif

Jana usiku Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alisema virusi vya corona vimeweka wazi ukweli kuhusu vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran. Amesema vikwazo vya Marekani ambavyo vimelenga afya ya Wairani ni ugaidi wa kiuchumi.

Katika ujumbe wake huo kwa munasaba wa siku kuu ya Nairuzi, Zarif amesema Marekani inalenga kuitenga Iran kupitia vikwazo lakini taifa la Iran kwa mara nyingine litasambaratisha vikwazo hivyo vya Marekani.