-
Kuakisiwa pakubwa shughuli ya kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani
Jan 07, 2020 09:43Mahudhurio ya jana ya mamilioni ya wananchi wa mji mkuu wa Iran, Tehran katika shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani pamoja na mashahidi wengine wa muqawama yameakisiwa pakubwa na vyombo vya habari katika eneo la Asia Magharibi na nje ya eneo hili.
-
Zarif: Mwisho wa uwepo wa shari wa Marekani Asia Magharibi umeanza
Jan 07, 2020 09:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa mwisho wa kuwepo kwa ushari Marekani katika eneo la Asia Magharibi umeanza na kueleza kuwa, taathira za kuuliwa kigaidi kiongozi wa kijeshi wa ngazi ya juu wa Iran zitaidhuru Marekani kwa kuchelewa au hivi karibuni kuanzia Mashariki hadi Magharibi.
-
Bin Alawi: Iran na Oman zinachukua hatua kwa ajili ya usalama wa eneo
Jan 07, 2020 08:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inachukua hatua kwa ajili ya kudhamini usalama wa eneo la Ghuba ya Uajemi na Oman pia inashirikiana na Tehran katika uwanja huo.
-
Shamkhani: Senario dhaifu zaidi ya kulipiza kisasi Iran; jinamizi la kihistoria kwa Marekani
Jan 07, 2020 08:48Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameitaja senario dhaifu zaidi ya kulipiza kisasi Iran kwa wale wote waliohusika na tukio la kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) kuwa litakuwa jinamizi la kihistoria kwa Marekani.
-
Kamanda wa IRGC: Tutalipiza kisasi cha kuuawa shahidi Jenerali Soleimani
Jan 07, 2020 04:46Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kisasi cha taifa la Iran kwa damu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha SEPAH kitakuwa kikali, madhubuti, cha kutisha na kamilifu.
-
Iran yakiongezea Kikosi cha Quds cha IRGC Yuro milioni 200
Jan 07, 2020 04:33Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ametangaza kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameidhinisha kukiongeza Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Yuro milioni 200.
-
Rais Hassan Rouhani ajibu vitisho vya Trump asema: 'Kamwe usilitishe taifa kubwa la Iran'
Jan 07, 2020 01:22Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa radiamali yake kufuatia vitsiho vya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu kuyalenga baadhi ya maeneo ya Iran kupitia ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, ambapo amemuonya kwa kusema: "Kamwe usilitishe taifa kubwa la Iran."
-
Zarif: Uwepo wa kishetani wa Marekani Asia Magharibi unaelekea kufika ukingoni
Jan 07, 2020 00:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria kujitokeza mamilioni ya Wairani katika mazishi ya mashahidi wa jinai ya hivi karibuni ya Marekani na kusema: "Uwepo wa kishetani wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi unaelekea kufika ukingoni."
-
Makumi ya watu wafariki dunia katika msongano Kerman, maziko ya Luteni Jenerali Soleimani yanaendelea
Jan 07, 2020 08:09Watu wasiopungua 52 wamefariki dunia mjini Kerman, Iran na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika mkanyagano kwenye shughuli ya kuuaga na kuusindikiza mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani pamoja na mashahidi wengine wa muqawama.
-
Bintiye Shahidi Soleimani: Jina la Haj Qassem Soleimani linawatia kiwewe Wazayuni, Wakufurishaji na Mabeberu
Jan 06, 2020 10:13Bintiye Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: "Baba yangu aliwakosesha usingizi madhalimu wote, madikteta na wakufurishaji. Jina la Haj Qassem Soleimani sasa pia linawatia kiwewe Wazayuni, wakufurishaji na mabeberu."