Kuakisiwa pakubwa shughuli ya kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58373-kuakisiwa_pakubwa_shughuli_ya_kuuaga_mwili_wa_luteni_jenerali_qassim_soleimani
Mahudhurio ya jana ya mamilioni ya wananchi wa mji mkuu wa Iran, Tehran katika shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani pamoja na mashahidi wengine wa muqawama yameakisiwa pakubwa na vyombo vya habari katika eneo la Asia Magharibi na nje ya eneo hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 07, 2020 09:43 UTC
  • Kuakisiwa pakubwa shughuli ya kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani

Mahudhurio ya jana ya mamilioni ya wananchi wa mji mkuu wa Iran, Tehran katika shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani pamoja na mashahidi wengine wa muqawama yameakisiwa pakubwa na vyombo vya habari katika eneo la Asia Magharibi na nje ya eneo hili.

Jana Jumatatu wakazi wa Tehran walitengeneza hamasa kubwa kutokana kwa kujitokeza kwa mamilioni na kuonyesha ni kwa kiasi gani wanawathamini mashujaa wa kitaifa. Hamasa hiyo kubwa imeakisiwa pakubwa na vyombo vya habari katika maeneo mbalimbali ya dunia vikiwemo vya Asia Magharibi ambavyo vimetumia ibara mbalimbali kuakisi tukio hilo la aina yake kama "Mawimbi Makubwa ya Wananchi", "Bahari ya Waombolezaji" na "Safu ya Kilomita Kadhaa ya Wairani". Kiujumla tunaweza kugawanya tathmini na uchambuzi wa tukio hilo katika makundi kadhaa.

Kundi Kwanza, limeyataja marasimu ya jana ya kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani na mashahidi wengine kuwa ni "tukio la kihistoria" na ni kwa sababu hiyo ndio maana limewashangaza na kuwaacha vinywa wazi. Mtandao wa Habari wa Times of Israel umeandika: Shughuli hiyo ya maombolezo na usindikizaji ni kubwa zaidi baada ya ile ya kuusindikiza mwili wa Imamu Khomeini.

Mashahidi Qassim Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandes

Kundi la Pili limesema kuwa, mahudhurio hayo makubwa yamedhihirisha umoja uliopo miongoni mwa wananchi. Mwandishi wa habari wa al-Monitor ameandika kuhusiana na suala hilo kwamba: Mimi sijawahi kushuhudia kitu kama hiki nchini Iran. Hata katika mikusanyiko na shughuli za kidini watu hawakusanyiki namna hii kama walivyojitokeza katika shughuli ya kumsindikiza na kumuaga Qassim Soleimani.

Kundi la Tatu limesisitiza kwamba, Luteni Jenerali Qassim Soleimani alikuwa mtu wa watu na alikuwa akipendwa mno. Mahudhurio hayo ya ya mamilioni watu siyo tu kwamba, yanaonyesha huba ya wananchi na hali yao ya kuthamini mchango wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani, bali yametoa pigo kwa vita vya kisaikolojia vya hivi karibuni vya vyombo vya habari vya kimataifa vilivyolenga kuharibu haiba ya kamanda huyu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH).

 

Kundi la Nne, limebainisha kwamba, mahudhurio hayo makubwa yamebainisha hisia ya chuki ya Wairani dhidi ya Marekani na wakati huo huo kuunga mkono "Kisasi Kikali" kilichoahidiwa na Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake wa rambirambi. Kanali ya Televisheni ya al-Jazeera ya Qatar sambamba na kuakisi shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani imeripoti kwamba, "matakwa ya kulipiza kisasi dhidi ya Marekani yameongezeka."

Kundi la Tano, limeyataja marasimu ya jana kwamba, ni fursa muhimu na ya aina yake kwa mwamko katika eneo la Asia Magharibi.

Kabla ya hapo pia, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon alitangaza kuwa, kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani ni "mwanzo wa historia mpya Asia Magharibi." Baada ya mahudhurio hayo ya mamilioni ya wananchi Vali Nasr mshauri ya Barack Obama Rais wa zamani wa Marekani ameandika: Angalia kikwango cha ushiriki wa waombolezaji katika shughuli ya kuuaga mwili wa Qassim Soleimani. Hii ni nukta muhimu katika Asia Magharibi.

Fauka ya hayo, marasimu ya jana mjini Tehran ya kuusindikiza mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani na mashahhidi wengine wa muqawama yameonyesha kuwa, kinyume na propaganda za vyombo vya habari vya kimataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina mtaji mkubwa wa rasilimali watu ambayo panapolazimu hujitokeza kwa wakati katika medani. Ukweli wa mambo ni kuwa, maombolezo na marasimu ya hivi karibuni katika miji wa Ahvaz, Mash'had, Qum, Tehran na Kerman yalikuwa ni "kura ya maoni" ya wananchi ya kuunga mkono mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.