Iran yakiongezea Kikosi cha Quds cha IRGC Yuro milioni 200
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58363-iran_yakiongezea_kikosi_cha_quds_cha_irgc_yuro_milioni_200
Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ametangaza kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameidhinisha kukiongeza Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Yuro milioni 200.
(last modified 2026-01-02T07:57:23+00:00 )
Jan 07, 2020 08:03 UTC
  • Iran yakiongezea Kikosi cha Quds cha IRGC Yuro milioni 200

Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ametangaza kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameidhinisha kukiongeza Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Yuro milioni 200.

Dakta Ali Larijani ametangaza katika kikao cha Bunge cha leo asubuhi kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, jana usiku aliidhinisha kutolewa fedha hizo kutoka kwenye Hazina ya Maendeleo ya Taifa kwa ajili ya Kikosi cha Quds cha SEPAH.

Aidha katika kikao hicho cha leo, Wabunge wa Iran wamepasisha kwa kauli moja hoja ya "Kisasi Kikali' ambayo itaandaa mazingira kwa Jamhuri ya Kiislamuya Iran kulipiza kisasi dhidi ya Washigton kwa kumuua shahidi Luteni Jenerali Qasse Soleimani, aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kadhalika Bunge la Iran limeangalia upya sheria iliyopasishwa Aprili mwaka jana, inayowatambua wanajeshi wote wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi (CENTCOM) na vikosi vyote vinavyofungamana nao kuwa kundi la kigaidi.

Bunge la Iran

Dakta Larijani amesema, "Hii leo, kufuatia hatua ya ukatili ya Marekani ya kumuua shahidi Jenerali Soleimani, huku Trump akibeba dhima na kukiri kuidhinisha mauaji hayo, tumeangalia upya sheria hiyo na kuanzia sasa, mbali na wanajeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi, Tehran itawatambua kama wanachama wa vikosi vya ugaidi wanachama wa Pentagon (Wizara ya Ulinzi ya Marekani), makamanda na maajenti wote wa Marekani waliohusika na mauaji hayo ya Jenerali Soleimani."

Bunge la Iran limehinikiza kwa nara za "Mauti kwa Marekani" baada ya kupasishwa hoja na miswada hiyo ya dharura ya kujibu chokochoko na ugaidi wa kiserikali wa Washington.