-
Iran: Miungano ya Marekani inasababisha machafuko kote ulimwenguni
Nov 09, 2019 10:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, miungano mbalimbali inayoundwa na Marekani inasababisha machafuko katika kona zote za dunia na kuhatarisha usalama na amani ya kila eneo lenye miungano hiyo.
-
Javad Larijani akosoa vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran
Nov 09, 2019 01:15Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu katika Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa kuendelea vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran.
-
Kamanda wa Jeshi la Anga la Iran: Tumetungua ndege isiyo na rubani ya nchi ya kigeni
Nov 08, 2019 23:45Kamanda wa Jeshi la Anga la Iran amesema kuwa jeshi hilo limetungua ndege isiyo na rubani ya nchi ya kigeni baada ya kuingia katika anga ya kusini mwa Iran katika eneo la Mahshahr.
-
Hatua ya Nne ya Iran; Kufeli 'Mashinikizo ya Juu Zaidi' ya Marekani
Nov 08, 2019 23:43Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: 'Marekani ni kinara wa shari, mwanzilishi na muungaji mkono wa ugaidi duniani."
-
Mtetemeko wa ardhi waua watu watano kaskazini magharibi mwa Iran
Nov 08, 2019 12:28Mtetemeko wa ardhi uliokuwa na ukubwa wa 5.9 kwa kipimo cha Rishta umetokea mapema leo Ijumaa katika wilaya ya Mianeh huko kaskazini magharibi mwa Iran na kuua watu wasiopungua 5.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Hasira ya Wairani dhidi ya Marekani ni ishara ya kukomaa kiakili
Nov 08, 2019 09:37Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa tangazo la hasira na chuki ya wananchi wa Iran dhidi ya ubeberu wa kimataifa unaoongozwa na Marekani ni kielelezo halisi cha umakini na kuwa macho mbele ya hatari kubwa inayotishia ubinadamu, amani na haki za binadamu.
-
Shamkhani: Haki za kisheria na maslahi ya wananchi wa Iran si mambo ya kujadiliwa
Nov 08, 2019 00:41Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza kuwa haki za kisheria na maslahi ya wananchi wa Iran si mambo ya kujadiliwa; na iwapo Marekani na nchi za Ulaya zitaendeleza mwenendo wa sasa zikiwa na matarajio kwamba Iran itasalimu amri bila shaka matokeo yake si jambo jingine ghairi ya majuto.
-
Kamanda Mkuu wa IRGC: Tutavigeuza vitisho vya adui kuwa fursa
Nov 07, 2019 09:39Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amewahutubu maadui wa taifa la Iran kwa kusema: 'Tutageuza kila vitisho mnavyovianzisha kuwa fursa na kusambaratisha kila lengo mnalofuatilia.
-
Hatua ya Nne ya Iran; kurutibishwa urani kwa kiwango cha asilimia 5 katika kituo cha Fordow
Nov 07, 2019 07:10Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameliagiza Shirika la Nishati ya Atomiki (IAEO) lianze kuingiza gesi kwenye mashinepewa (centrifuges) katika kituo cha nyuklia cha Fordow, ikiwa ni katika utekelezaji wa hatua ya nne ya kupunguza uwajibikaji wa Tehran katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Zoezi la urutubishaji na uzalishaji mpya wa urani katika kituo cha Fordow waanza rasmi nchini Iran
Nov 07, 2019 03:41Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa, mapema leo asubuhi, limeanza zoezi la kurutubishwa na kuzalishwa upya urani katika kituo cha nyuklia cha Shahid Ali Mohammadi, maarufu kwa jina la Fordow, kaskazini mashariki mwa mji wa Qum wa kusini mwa Tehran.