-
Rais Rouhani: Taifa la Iran limesimama imara kukabiliana na Marekani
Oct 19, 2019 23:32Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa la Iran limesimama imara na kwa nguvu zote katika miaka mingi sasa kukabiliana na ubeberu wa Marekani na kwamba Marekani na mabeberu wenzake pamoja na vibaraka wao kamwe hawawezi kulipigisha magoti taifa hili la Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Kusimama kidete katika njia iliyonyooka, ni kwa maslahi ya taifa na dunia
Oct 19, 2019 09:53Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kusimama kidete katika njia iliyonyooka na ya haki, ni kwa maslahi ya taifa la Iran na dunia yote kwa ujumla.
-
Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS, mjumuiko kwa ajili ya uhuru na kuwatetea waliodhulumiwa
Oct 19, 2019 08:37Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametembelea vibanda vya kuwahudumia wafanyaziara (Mawkib) katika kituo cha mpakani cha Chazabeh kusini magharibi mwa Iran na akizugumza na waandishi habari amesema, matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS ni mhimili wa kutaka uhuru na kutetea watu wa Palestina na pia ni mjumuiko dhidi ya Uzayuni.
-
Matembezi makubwa ya "Waliosalia Nyuma" katika Arubaini ya Imam Hussein (as) yafanyika mjini Tehran
Oct 19, 2019 04:33Matembezi ya "Waliosalia Nyuma" katika Arubaini ya Imam Hussein (as) yamefanyika katika mwendo wa kilomita 17 kuanzia kwenye medani ya Imam Hussein (as) hapa mjini Tehran kuelekea haram ya mtukufu Abdul-Adhim (as) iliyoko mjini Rey kusini mwa Tehran kwa kuhudhuriwa na wapenzi na maashiki wa Imam Hussein (as).
-
Jahangiri: Arubaini ya Imam Hussein (as) ni dhihirisho la mshikamano na umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu
Oct 19, 2019 03:53Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhudhuria mamilioni ya maashiki wa Imam Hussein (as) kutoka madhehebu, dini na nchi mbali mbali na kukusanyika pamoja kwa kipindi kifupi ni dhihirisho la upendo, mshikamano na umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu.
-
Mamilioni wakusanyika Karbala katika Arubaini ya Imam Hussein (as)
Oct 18, 2019 13:20Mamilioni ya Waislamu wanakusanyika katika mji mtakatifu wa Karbaka nchini Iraq kwa ajili ya kushiriki katika shughuli ya Arubaini ya Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (as).
-
Shamkhani: Hakuna nchi inayoweza kudhuru usalama wa Iran
Oct 18, 2019 13:11Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameashiria uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa hakuna nchi inayoweza kuusababishia madhara usalama wa Iran.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Matembezi ya Arubaini yamekuwa jinamizi kwa maadui
Oct 18, 2019 11:52Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema, Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein (as) ni safu za wapigania uhuru duniani wanaokabiliana na maadui; na akaongeza kwamba: Matembezi ya Arubaini yamegeuka kuwa jinamizi kwa maadui.
-
"Iran haitakuwa mtekelezaji pekee wa makubaliano ya nyuklia"
Oct 17, 2019 23:56Naibu Balozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Tehran haipaswi kuwa mtekelezaji pekee wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA iwapo upande wa pili hautatekeleza wajibu wake.
-
Iran: Kuzinduliwa ndege mpya ya kivita ya Yasin, ishara ya kushindwa vikwazo
Oct 17, 2019 10:03Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya Iran kuzindua ndege mpya ya kivita iliyotengenezwa na wataalamu wa kijeshi wa hapa nchini ni ishara tosha kuwa vikwazo vya kidhalimu vya Marekani havijakuwa na athari zozote kwa taifa hili.