-
Iran: Kuzinduliwa ndege mpya ya kivita ya Yasin, ishara ya kushindwa vikwazo
Oct 17, 2019 10:03Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya Iran kuzindua ndege mpya ya kivita iliyotengenezwa na wataalamu wa kijeshi wa hapa nchini ni ishara tosha kuwa vikwazo vya kidhalimu vya Marekani havijakuwa na athari zozote kwa taifa hili.
-
Rouhani: Kuimarishwa uhusiano wa Iran na Afrika Kusini ni kwa manufaa ya nchi mbili
Oct 17, 2019 04:44Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran usiku wa kuamkia leo ameonana na Naledi Pandor, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini hapa Tehran na kutilia mkazo udharura wa kustawisha ushirikiano wa pande zote baina ya nchi mbili akisisitiza kuwa, kustawishwa uhusiano huo ni kwa manufaa ya nchi zote mbili na maeneo yao.
-
Larijani: Nchi nyingi zina hamu ya kuwa na uhusiano mzuri wa kiuchumi na Iran
Oct 17, 2019 04:30Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge kla Iran) amesema kuwa, viongozi wa nchi nyingi wanachama wa Umoja baina ya Mabunge Duniani wanailaumu Marekani kwa kutoheshimu ahadi zake ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na wana hamu ya kuwa na uhusiano mzuri wa kiuchumi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Zarif: Ulaya imeshindwa kutekeleza majukumu yake ndani ya JCPOA
Oct 16, 2019 22:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Ulaya imeshindwa kutekeleza majukumu yake ndani ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na iwapo pande husika katika makubaliano hayo hazitayatekeleza, Iran itachukua hatua za dharura za kupunguza utekelezaji wa mapatano hayo ya nyuklia.
-
Rais Rouhani: Iran imeendelea katika teknolojia na taaluma mbalimbali
Oct 16, 2019 08:54Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba nchi hii imeendelea katika elimu na taaluma tofauti amesema kuwa, licha ya matatizo ambayo yameikabili Iran katika kipindi cha miaka 40 iliyopita vikiwemo vita vya kulazimishwa na mashanikizo ya kiuchumi, lakini vyuo vikuu vimetekeleza vizuri majukumu yao.
-
Zarif ataka kusitishwa uvamizi wa kijeshi dhidi ya Syria
Oct 16, 2019 04:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito wa kusitishwa uvamizi na mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria.
-
Tehran ni mwenyeji wa mkutano wa Mawaziri wa Afya wa Nchi za Eneo la Mediterania Mashariki
Oct 16, 2019 03:53Hatua ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA ni fedheha kwa Marekani na fedheha kubwa zaidi kwa nchi hiyo ni kuwawekea watu wa Iran vikwazo vya dawa na chakula.
-
Rouhani: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran ni ugaidi wa kiuchumi
Oct 15, 2019 09:40Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, hatua ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA ni fedheha kwa Marekani na kuongeza kuwa: "Fedheha kubwa zaidi kwa Marekani ni kuwawekea watu wa Iran vikwazo vya dawa na chakula."
-
Zarif: Kushambuliwa meli ya mafuta ya Iran kulitekelezwa na serikali moja au kadhaa
Oct 15, 2019 09:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia, shambulizi dhidi ya meli ya mafuta ya Iran inayojulikana kama SABITI lilitekelezwa na serikali moja au serikali kadhaa.
-
Larijani: Suala la Palestina limepuuzwa kutokana na hali ya mchafukoge katika Ulimwengu wa Kiislamu
Oct 15, 2019 04:15Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, suala la Palestina linapuuzwa kutokana na hali ya mchafukoge inayoshuhudiwa katika Ulimwengu wa Kiislamu na akasisitiza kuwa: Umoja wa Mabunge ya Nchi za Kiislamu unapaswa kuwa sauti ya wazi ya kuisemea Palestina.