Rais Rouhani: Iran imeendelea katika teknolojia na taaluma mbalimbali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56662-rais_rouhani_iran_imeendelea_katika_teknolojia_na_taaluma_mbalimbali
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba nchi hii imeendelea katika elimu na taaluma tofauti amesema kuwa, licha ya matatizo ambayo yameikabili Iran katika kipindi cha miaka 40 iliyopita vikiwemo vita vya kulazimishwa na mashanikizo ya kiuchumi, lakini vyuo vikuu vimetekeleza vizuri majukumu yao.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 16, 2019 08:54 UTC
  • Rais Rouhani: Iran imeendelea katika teknolojia na taaluma mbalimbali

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba nchi hii imeendelea katika elimu na taaluma tofauti amesema kuwa, licha ya matatizo ambayo yameikabili Iran katika kipindi cha miaka 40 iliyopita vikiwemo vita vya kulazimishwa na mashanikizo ya kiuchumi, lakini vyuo vikuu vimetekeleza vizuri majukumu yao.

Rais Rouhani ameyasema hayo sambamba na kuanza rasmi muhula wa masomo wa vyuo vikuu na vituo vya utafiti na taknolojia nchini katika Chuo Kikuu cha Tehran na kuongeza kuwa, hii leo kiwango cha vyuo vikuu nchini Iran kikilinganishwa na eneo zima la Asia Magharibi na hata nchi zilizoendelea, ni cha kuridhisha na vinaendelea kupata mafanikio makubwa katika nyanja za kielimu na maarifa. Akiashiria kwamba mabadiliko ya sasa duniani yanakwenda kwa kasi kubwa amebainisha kuwa, vyuo vikuu vya Iran vinapasa kuwalea wanachuo wao kwa ajili ya mustakbali bora wa baadaye. 

Maendeleo mbalimbali ya kielimu nchini Iran licha ya kuwepo vikwazo

Huku akisisitiza kuwa Iran iko tayari kushirikiana na nchi tofauti, Rais Hassan Rouhani amesema kuwa, ushirikiano huo hauna maana kwamba Iran inaposhambuliwa, basi ikae kimya na kutochukua hatua yoyote ya kujitetea. Kadhalika Rais Rouhani ameashiria kukaribia uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (yaani bunge) na kusema kuwa, njia bora ya kurekebisha jamii, ni kupitia masanduku ya kupigia kura.