-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Sutafahamu zilizotokea baina yetu na Qatar zimeondolewa
Sep 05, 2025 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema, mazungumzo yake na viongozi wa Qatar yalikuwa yenye faida na mafanikio makubwa na yalifanyika kwa uzito maalumu na akaongezea kwa kusema: "kwa bahati nzuri, hakuna tofauti zozote kati ya nchi hizi mbili, na sutafahamu iliyojitokeza imetatuliwa kikamilifu na ziara hii".
-
"Hatua ya nchi za Ulaya kuamilisha utaratibu wa snapback ni ya kiholela"
Sep 05, 2025 08:38Khatibu wa Muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswalia leo hapa Tehran amesema: Kwa mujibu wa taarifa ya mwisho ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, jaribio lolote la kubadilisha Azimio Nambari 2231 linadhoofisha itibari ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwamba hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuamilisha utaratibu wa "snapback" wa kurejesha vikwazo vya baraza hilo dhidi ya Iran ni ya kiholela.
-
IRGC: Adui hana ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran
Sep 05, 2025 07:33Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema Israel na washirika wake hawana uwezo wala ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran, hivyo basi, wamekimbilia operesheni za vita vya kisaikolojia.
-
Iran yaitaka dunia ilaani mashambulizi dhidi ya vituo vyake vya nyuklia
Sep 05, 2025 07:32Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Iran amesema Marekani na utawala wa Israel zilifanya mashambulizi ya kimakusudi dhidi ya vituo vya nyuklia ya Iran, licha ya vituo hivyo kuwa chini ya usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Nyuklia.
-
Araqchi: 'Iran itaendelea kuunga mkono Muqawama wa Palestina dhidi ya Israel'
Sep 05, 2025 03:37Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesisitiza dhamira ya nchi hiyo ya kuunga mkono Muqawama halali na mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya utawala vamizi wa Israel hadi pale haki zao zitakaporejeshwa kikamilifu.
-
Ripoti: Takriban Wairani 100 walikuwa wahanga wa ugaidi katika mwaka uliopita wa Kiajemi
Sep 04, 2025 22:52Mashambulizi ya kigaidi yaligharimu maisha ya takriban Wairani mia moja katika mwaka uliopita wa kalenda ya Kiirani, uliomalizika Machi 20. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika lisilo la kiserikali linalowakilisha familia za wahanga Wairani wa mashambulizi ya kigaidi.
-
Araqchi: IAEA imeafiki haja ya mfumo mpya wa ushirikiano na Iran
Sep 04, 2025 22:49Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa hakutakuwa na ushirikiano mpya baina ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) hadi hapo mazungumzo yatakapokamilika.
-
Iran yalipiza kisasi: Balozi wa Australia aondoka Tehran
Sep 04, 2025 11:12Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametangaza kwamba balozi wa Australia mjini Tehran ameondoka nchini na kuongeza kuwa: "Kwa mujibu wa kaida na sheria za kidiplomasia, katika kukabiliana na hatua ya Australia ya kumfukuza balozi wa Iran mjini Canbera, Jamhuri ya Kiislamu imejibu mapigo kwa kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia wa Australia nchini Iran."
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Jumuiya ya Shanghai inaweza kuasisi miungano ya usalama yenye ufanisi
Sep 04, 2025 10:33Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amesema kuwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ina uwezo wa kupanua wigo wa shughuli zake na kuanzisha miungano ya usalama yenye ufanisi katika siku zijazo.
-
Araghchi: Iran haiogopi mazungumzo, wala vita
Sep 04, 2025 04:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu haiogopi kuingia katika mazungumzo mapya kuhusu utatuzi wa masuala yoyote yaliyopo, kama ambavyo haina hofu ya kuingia katika vita vyovyote vipya ambavyo vinaweza kutwishwa nchi hii na maadui zake.