-
Wapalestina 127 wameshakufa shahidi kutokana na njaa na lisheduni katika Ukanda wa Ghaza
Jul 27, 2025 07:38Maafisa wa utoaji misaada katika Ukanda wa Ghaza wametangaza leo kuwa watu 127 wamekufa shahidi kwa utapiamlo na njaa kutokana na mzingiro mkubwa lililowekewa eneo hilo na utawala wa kizayuni na hatua ya utawala huo ghasibu ya kuzuia uingizaji misaada ya kibinadamu.
-
Nini uchambuzi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki kuhusu lengo la utawala wa Kizayuni huko Gaza?
Jul 27, 2025 06:47Hakan Fidan Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ametahadharisha kuhusu nia ya utawala wa Kizayuni ya kuwaondoa wakaazi wa Gaza kutoka katika ukanda huo.
-
Ndege ya kijeshi ya mizigo ya US yatua kwenye kituo cha kaskazini ya mkoa wa Hasakah, Syria
Jul 27, 2025 06:25Duru za Syria zimeripoti kuwa ndege ya kijeshi ya Marekani ya mizigo imetua kaskazini mwa mkoa wa Hasakah.
-
Jeshi la Majini la Israel lateka meli ya msaada iliyokuwa ikielekea Gaza
Jul 27, 2025 03:51Jeshi la majini la utawala ghasibu wa Israel limeiteka meli ya misaada iliyokuwa ikielekea Ukanda wa Gaza, ikiwa na bendera ya Uingereza, katika harakati za kuvunja mzingiro mkali wa eneo hilo unaoendelea tangu mwaka 2007.
-
Familia ya Kipalestina yalazimika kula majani ya mti kutokana na kukosa chakula
Jul 26, 2025 23:47Maafa ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza huko Palestina yamefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, ambapo watu waliozingirwa na uhaba mkubwa wa chakula wanalazimika kula majani ya mti ili kukidhi njaa yao.
-
Msalaba Mwekundu: Viwango vyote vya kisheria na kimaadili vimekiukwa huko Gaza
Jul 26, 2025 23:06Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu amezungumzia hali mbaya ya inayoshuhudiwa sasa katika Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi ya jeshi la Israel na mzingiro mkubwa wa eneo hilo na kusisitiza kuwa, viwango vyote vya kisheria na kimaadili vimekiukwa katika Ukanda wa Gaza.
-
Hamas yaijibu Marekani kuhusu usitishaji mapigano, yamtaja Netanyahu kuwa ndiye kizuizi cha amani
Jul 26, 2025 23:05Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imewashutumu maafisa wa serikali ya Marekani kwa kupotosha umma kuhusu msimamo ya harakati hiyo katika mazungumzo ya kusitisha mapigano, na kulitaja baraza la mawaziri la Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuwa ndio kikwazo kikuu cha kufikiwa usitishaji mapigano.
-
Kwa nini umoja wa nchi za Kiislamu ni jambo la dharura kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Gaza?
Jul 26, 2025 22:56Sayyid Abbas Araqchiو Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni Israel katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, kuna haja ya kuchukuliwa hatua haraka na nchi za Kiislamu kufanya uratibu ili kusitisha mauaji ya kimbari na kuzuia maafa ya binadamu yanayoendelea huko Gaza.
-
Haaretz: Israel iliua watoto 1,000 wa Kipalestina mwezi uliopita
Jul 26, 2025 08:06Gazeti la Kizayuni la "Haaretz" limekiri Jumamosi ya leo kwamba, jeshi la utawala huo liliua watoto 1,000 katika mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza mwezi uliopita pekee.
-
Ayatullah Sistani: Mataifa ya Kiarabu na Kiislamu yachukue hatua kukabiliana na njaa kali Gaza
Jul 26, 2025 04:28Kiongozi mkuu Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, ameelezea masikitiko yake makubwa kuhusu hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota katika Ukanda wa Gaza, hususan baa la njaa linalozidi kushika kasi, na kutoa wito kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za haraka kukomesha janga hili la kusikitisha.