-
Ripoti: Israel imeua wanahabari wa Kipalestina 212 tangu Oktoba, 2023
Apr 25, 2025 23:08Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Gaza imesema, kutokana na mauaji ya mwanahabari Saeed Amin Abu Hassanein, idadi ya waandishi wa habari wa Palestina waliouawa shahidi na Israel imeongezeka hadi 212, tangu vita vya mauaji ya kimbari vilipoanza katika eneo hilo lililozingirwa mnamo Oktoba mwaka 2023.
-
Rais wa Misri kwa mara nyingine apinga kuhamishwa Wapalestina Gaza
Apr 25, 2025 23:08Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi jana Ijumaa alisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba nchi hiyo ya Kiarabu "inapinga kikamilifu" kufurushwa Wapalestina kwenye makazi yao na kuhamishiwa katika nchi nyingine, na kuvitaja vita vya Gaza kuwa "janga la kibinadamu."
-
AP: Yemen imetungua droni 7 za US zenye thamani ya dola milioni 200
Apr 25, 2025 23:07Vikosi vya Yemen vimetungua ndege saba zisizo na rubani za Marekani aina ya Reaper katika kipindi cha chini ya wiki sita, na kuisababishia Washington hasara ya zaidi ya dola milioni 200.
-
Mashambulio ya kinyama ya Israel yaua Wapalestina wengine 60 Ghaza, 12 wanatoka familia moja
Apr 25, 2025 04:11Zaidi ya watu 60 wameuawa shahidi katika mashambulio ya kinyama ya karibuni zaidi kufanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka.
-
Mhariri Mkuu wa Middle East Eye: Harakati ya HAMAS katu haitasalimu amri
Apr 25, 2025 03:53David Hearst, Mhariri Mkuu wa tovuti ya habari ya Middle East Eye amesema, Muqawama ndio njia pekee iliyobaki kwa ajili ya kukomesha ughasibu na kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Al-Jolani: Syria iko tayari kuanzisha uhusiano rasmi na Israel 'kwa masharti sahihi'
Apr 25, 2025 03:32Rais wa mpito wa Syria Al-Jolani amesema yuko tayari kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel. Hayo ni kwa mujibu wa barua inayoripotiwa kuwa ameituma kwa Rais wa Marekani Donald Trump.
-
Kuendelea jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza mbele ya kimya cha wanaodai kutetea haki za binadamu
Apr 24, 2025 06:39Umoja wa Mataifa umesema kukwa umekumbwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza na kutahadharisha kuwa eneo hilo linapitia katika hali ngumu sana tangu kuanza vita dhidi ya ukanda huo.
-
Iraq: Tunaunga mkono mazungumzo ya Iran na Marekani
Apr 24, 2025 03:59Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq Fuad Hussein amesema kuwa, nchi yake inaunga mkono mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani.
-
UN: Hali ya kibinadamu Gaza ni mbaya zaidi tangu vita vilipoanza
Apr 24, 2025 03:58Msemaji wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) ameeleza wasi wasi wake mkubwa juu ya hatua ya utawala wa Israel ya kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza na kubainisha kwamba, hali ya sasa ya Ukanda huo ni mbaya zaidi tangu kuanza kwa vita hivyo.
-
Serikali ya Jordan yaipiga marufuku harakati kongwe ya Kiislamu ya Ikhwanul-Muslimin
Apr 24, 2025 00:44Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jordan ametangaza kuwa utawala huo wa kifalme umeipiga marufuku harakati ya Kiislamu ya Ikhwanul-Muslimin na kuielezea "itikadi" yake inayohubiri kuwa sasa ni 'haramu' kisheria nchini humo.