-
Hilali Nyekundu ya Palestina: Ripoti ya Israel ya mauaji ya wahudumu wa tiba 'imejaa uwongo'
Apr 21, 2025 03:45Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina limekanusha vikali ripoti ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu mauaji liliyofanya mwezi uliopita ya zaidi ya wafanyakazi 15 wahudumu wa sekta ya tiba huko Ghaza, ambayo utawala huo umedai waliuawa kimakosa.
-
Muqawama Iraq: Huenda kongozi wa Hayat Tahrir al-Sham ya Syria akamatwa akija Baghdad
Apr 20, 2025 22:55Kiongozi wa kundi la Muqawama na kupambana na ugaidi la Asa’ib Ahl al-Haq nchini Iraq ameonya kwamba, anayejiita rais wa Syria Abu Mohammed al-Jolani anaweza kukamatwa atakapowasili Baghdad, kutokana na kuwepo hati ya kukamatwa kwake.
-
Misafara ya askari, silaha za Marekani yaingia Ain al-Asad, Iraq ikitokea Syria
Apr 20, 2025 22:54Jeshi la Marekani limeripotiwa kutuma misafara mingi ya malori yaliyobeba wanajeshi, silaha na zana kivita, pamoja na suhula za kilojistiki kutoka ndani kabisa ya Syria hadi katika kambi kubwa ya anga ya Ain al-Asad katika jimbo la Anbar nchini Iraq, ambayo ina wanajeshi na wakufunzi wa Marekani.
-
Qatar yalaani mpango wa Wazayuni wa kubomoa Msikiti wa Al-Aqswa
Apr 20, 2025 22:52Qatar imelaani vikali mpango wa taasisi za Wazayuni wenye misimamo mikali ya kubomoa msikiti wa Al-Aqswa katika mji wa Baytul-Muqaddas.
-
Wapalestina 18 wauawa shahidi katika unyama mwingine wa Israel
Apr 20, 2025 08:38Mashambulizi ya leo ya utawala haramu wa Israel katika maeneo mbalimbali ya Gaza yamesababisha vifo vya watu 18 na wengi kujeruhiwa.
-
Palestina: Walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya chuki wanachochea Msikiti wa Al-Aqsa uripuliwe
Apr 20, 2025 02:03Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetoa indhari kutokana na kuongezeka uchochezi unaofanywa na makundi ya walowezi wa Kizayuni wa mrengo wa kulia wanaotaka kubomolewa Msikiti wa Al-Aqsa ulioko Baitul-Muqaddas Mashariki inayokaliwa kwa mabavu.
-
Wagonjwa laki mbili hatarini kufariki dunia Ghaza kutokana na Israel kuendelea kufunga vivuko
Apr 19, 2025 22:56Wizara ya Afya ya Palestina imetahadharisha kuwa watu 200,000 wenye maradhi thakili wako hatarini kupoteza maisha kutokana na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuendelea kuvifunga vivuko, jambo ambalo linavuruga pia utendaji kazi wa hospitali katika Ukanda huo.
-
Mkuu wa Umoja wa Maulamaa aghadhibishwa vikali na kimya cha Ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na Ghaza
Apr 19, 2025 22:54Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu amekosoa vikali kimya cha Ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Waislamu Wapalestina wa Ghaza.
-
Muqawama wa Ghaza watoa pigo jingine, waangamiza na kujeruhi Wazayuni 6
Apr 19, 2025 09:43Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimeripoti "tukio kubwa la usalama" katika Ukanda wa Ghaza na pigo jingine jipya kutoka kwa Muqawama dhidi ya wanajeshi vamizi wa Israel.
-
Iran yataka kusitishwa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa mashambulizi ya Marekani huko Yemen
Apr 18, 2025 22:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu iko bega kwa bega na wananchi wanamapambano wa Yemen na ametoa wito wa kukomeshwa kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya ukiukwaji wa wazi wa sheria za kibinadamu na kanuni za kimataifa unaofanywa na Marekani dhidi ya watu wa Yemen.