-
Ansarullah: US inashajiisha mauaji ya kimbari Gaza, yataka Wapalestina wapewe silaha
Apr 18, 2025 03:00Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani inaihimiza na kuishajiisha Israel kuendeleza vita vya mauaji ya halaiki huko Gaza na kusisitiza kuwa Washington ni mshiriki wa utawala wa Kizayuni katika mauaji hayo ya kimbari.
-
Mashambulizi ya anga ya US kwenye bandari ya mafuta ya Ras Isa, Yemen yaua watu 33
Apr 17, 2025 23:33Jeshi la Marekani limeshambulia bandari ya mafuta ya Ras Isa magharibi mwa Yemen, na kuua makumi ya wafanyakazi na wahudumu wa afya, huku makumi ya wengine wakijeruhiwa.
-
Taasisi ya Palestina: Siku ya mateka wa Palestina; nembo ya mapambano yao katika jela za Israel
Apr 17, 2025 23:10Ofisi ya Habari ya serikali katika Ukanda wa Gaza imetaja tarehe 17 Aprili liyoadhimishwa jana Alhamisi ambayo imepewa jina la Siku ya Mateka wa Palestina kuwa ni inakumbusha mateso, maumivu na masaibu wanayopitia zaidi ya mateka elfu kumi wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni.
-
HAMAS yakataa pendekezo la kuweka silaha chini
Apr 17, 2025 09:10Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeripotiwa kupinga pendekezo la utawala haramu wa Israel la kusitisha vita kwa muda wa wiki sita katika Ukanda Gaza, sambamba na kulitaka kundi hilo la muqawama kuafiki kupokonywa silaha.
-
Jasusi mzoa taka anaswa kwenye mtego wa vikosi vya Muqawama Ghaza
Apr 17, 2025 02:12Vikosi vya Muqawama huko Ghaza vimemnasa kwenye mtego, jasusi wa utawala katili wa Kizayuni wa Israel ambaye alijifanya ni mzoa taka kumbe alikuwa anafanya ujasusi wa kujua walipo mateka wa Kizayuni.
-
Hamas yaitisha maandamano ya 'mshikamano wa kimataifa' kulaani jinai za Israel Gaza
Apr 16, 2025 23:01Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa wito wa dharura kwa watu wa dunia kushiriki kikamilifu katika maandamano ya wiki moja ya kushinikiza kusitishwa kwa kampeni ya kutisha ya Israel ya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.
-
Saudi Arabia yaanzisha tena mashambulizi dhidi ya Yemen?
Apr 16, 2025 23:00Vyanzo vya ndani nchini Yemen vimeripoti habari ya kujiri mashambulizi ya mizinga na makombora ya Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo jirani yake.
-
Makumi ya wanawake, watoto wauawa na mabomu ya Wazayuni Gaza
Apr 16, 2025 11:21Mashambulizi makali ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel yameua shahidi zaidi ya Wapalestina 20, wakiwemo wanawake na watoto wadogo katika Ukanda wa Gaza.
-
Serikali ya Al-Jolani Syria kuanzisha uhusiano rasmi na Israel mwishoni mwa 2026
Apr 16, 2025 08:02Mwanadiplomasia mmoja wa Uingereza amefichua kuwa kiongozi wa kundi la wanamgambo la Hay-at Tahrir al-Sham HTS Abu Mohammed al-Jolani ameihakikishia Uingereza kwamba Syria "itaanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia" na utawala wa Kizayuni wa Israel, itautambua utawala huo, na kubadilishana nao mabalozi ifikapo mwisho wa mwaka ujao wa 2026.
-
UAE imeweka mtambo wa rada wa Israel Puntland kwa ajili ya kutungua makombora ya Yemen
Apr 16, 2025 08:01Duru za habari zimeripoti kuwa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) au Imarati imeweka mtambo wa rada wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Puntland, Somalia ili kuyanasa na kuyatungua makombora yanayorushwa na Yemen.