-
Jeshi katili la Israel laendelea kumwaga damu za Wapalestina Gaza
Mar 24, 2025 23:21Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina wengine 17 katika mashambulizi ya alfajiri ya leo katika Ukanda wa Gaza, siku moja baada ya kuua shahidi Wapalestina zaidi ya 60 akiwemo ripota wa Al Jazeera, Hossam Shabat katika ukanda huo.
-
Umuhimu wa msimamo wa kamati ya mawaziri wa nchi za Kiarabu na Kiislamu dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza.
Mar 24, 2025 22:49Kamati ya Mawaziri ya Nchi za Kiarabu na Kiislamu imeelezea wasi wasi wake kuhusu mashambulizi mapya ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kutaka kutekelezwa mara moja na kikamilifu usitishaji vita kwa mujibu wa azimio nambari 2735 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Chombo cha Kizayuni: Kuna ukosefu wa kuaminiana kitaasisi Israel
Mar 24, 2025 07:22Chombo kimoja cha habari cha lugha ya Kiebrania kimechapisha makala inayofichua mzozo mkubwa wa kutoaminiana ndani ya muundo wa mamlaka na kiutawala huko Israel.
-
Siku ya saba ya uvamizi wa Israel wa Ghaza; makumi wauawa na kujeruhiwa
Mar 24, 2025 07:21Utawala wa wa Kizayuni wa Israel Israel unaendelea kufanya jinai na mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza ambapo tangu asubuhi ya leo hadi wakati tunaandaa taarifa hii, makumi ya Wapalestina wamekuwa wameshauwa shahidi na kujeruhiwa, leo ikiwa ni siku ya saba ya tangu kuanza wimbi jipya la jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza.
-
Hamas; kuuawa shahidi Barhoum; jinai nyingine katika rekodi nyeusi ya utawala wa Kizayuni
Mar 24, 2025 04:37Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa taarifa na kutoa mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi Esmail Barhoum mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo.
-
Mchambuzi: Kurukia vita baada ya vita ni 'muhimu' kwa Netanyahu kubaki madarakani
Mar 23, 2025 23:01Elijah Magnier, mchambuzi mashuhuri wa masuala ya kijeshi amesema, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu anafanya juu chini ili aweze kusalia madarakani kwa angalau miaka miwili mingine; na hiyo ndiyo sababu ya "kurukia vita baada ya vita".
-
Hamas: Mauaji ya Wapalestina akiwemo Mbunge yataimarisha Muqawama
Mar 23, 2025 07:29Jeshi la Israel limefanya mashambulizi mapya ya kutisha ya anga katika Ukanda wa Gaza na kuua shahidi watu wasiopungua 40, akiwemo Salah al-Bardawil, Mbunge wa Palestina na Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas.
-
Israel yapigwa na makombora kutoka Yemen, ving'ora vyahanikiza
Mar 23, 2025 07:21Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimevurumisha makombora kuelekea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, na kuwatia kiwewe na hofu Wazayuni; huku safari za ndege zikisimamishwa Tel Aviv.
-
Hamas: Muqawama ni chaguo la kimkakati la ukombozi wa Palestina
Mar 23, 2025 03:03Katika kumbukumbu ya mwaka wa 21 wa kuuawa shahidi Sheikh Ahmad Yassin, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kwa kusema: "Tunashikamana na njia ya Sheikh Ahmad Yassin, tunalinda ardhi na matukufu yetu, na tuna imani thabiti kwamba Muqawama ni chaguo la kistratijia la kujikomboa na kupata uhuru wetu."
-
Hizbullah yapinga madai ya kuhusika na shambulio la maroketi
Mar 22, 2025 23:18Baada ya utawala wa Israel kudai kwamba maroketi 5 yalirushwa kuelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu jana Jumamosi, Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imekanusha kuhusika kivyovyote na shambulio hilo.