-
Hamas: Washington inabeba dhima ya kifo cha mwanajeshi aliyejichoma moto nje ya Ubalozi wa Israel huko Washington + video
Feb 27, 2024 09:13Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema serikali ya Marekani inabeba dhima ya kifo cha mwanajeshi wa nchi hiyo aliyejichoma moto nje ya Ubalozi wa Israel huko Washington akipinga uungaji mkono wa serikali ya Rais Joe Biden kwa mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel huko Ukanda wa Gaza.
-
Yemen: Mashambulizi katika Bahari ya Sham yatakoma pale tu Israel itakapositisha vita Gaza
Feb 27, 2024 23:22Msemaji wa Harakati ya Ansarullah inayotawala Yemen amesema mashambulizi ya nchi hiyo ya Kiarabu dhidi ya meli za maadui katika Bahari ya Sham yatakoma tu baada ya utawala wa Israel kuhitimisha vita na mzingiro wake dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
OIC yaziomba nchi zote duniani zisiuuzie silaha utawala wa Kizayuni wa Israel
Feb 27, 2024 07:50Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amezitaka nchi zote duniani kuacha kutuma silaha na zana za kijeshi kwa utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel.
-
HAMAS: Historia katu haitasahau hatua za fedheha za Biden
Feb 27, 2024 03:57Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema historia kamwe haiwezi kufuta hatua ya kufedhehesha ya utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani ya kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mauaji yake ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Kauli moja ya mirengo ya kisiasa ya Iraq kuhusu wajibu wa kuondoka wanajeshi wa kigeni nchini mwao
Feb 26, 2024 23:01Qasim al-Araji, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Iraq amesisitiza kuwa mirengo yote ya kisiasa ya nchi hiyo yanakubaliana kwa kauli moja kuhusu wajibu wa kuondoka wanajeshi wa kigeni nchini humo.
-
Mkuu wa UNRWA: Janga la njaa la 'kutengezwa na watu' Ghazza linaepukika kwa kuruhusu kuingizwa misaada
Feb 26, 2024 08:17Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amesema baa la njaa kali lililozagaa katika Ukanda wa Gaza linaweza kuepukwa ikiwa misaada itaruhusiwa kuingizwa katika eneo hilo.
-
Waziri wa Ulinzi wa Yemen: Zama za Marekani na waitifaki wake 'kuhodhi' maji ya kimataifa zimekwisha
Feb 26, 2024 07:58Waziri wa Ulinzi wa Yemen amepongeza operesheni za majini zinazoendelea kufanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya meli zenye uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Bahari Nyekundu kwa lengo la kupinga vita dhidi ya Ghazza, na kusisitiza kwamba zama za "satua ya kuhodhi" Marekani na washirika wake maji ya kimataifa zimekwisha.
-
Waziri Mkuu wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ajiuzulu
Feb 26, 2024 07:53Waziri Mkuu wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mohammad Ashtiyah, amejiuzulu wadhifa wake huo.
-
Kuendelezwa mauaji ya halaiki ya jeshi la Israel katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza
Feb 26, 2024 03:45Wapalestina wengine wameuawa shahidi kufuatia mashambulizi ya anga na mizinga ya jeshi katili la Israel linaloendeleza mauaji ya kimabari katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza.
-
OIC yailaani Israel kwa mauaji ya kimbari ya raia Wapalestina Gaza
Feb 26, 2024 03:15Mawaziri wa habari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wamelaani "ukandamizaji wa kimfumo na mauaji ya kimbari ya raia wa Palestina" huko Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.