-
Kundi la kwanza la Wapalestina wanaorejea kutoka Misri lapitia kivuko cha Rafah
Feb 02, 2026 10:24Kundi la kwanza la Wapalestina limeanza kurejea katika Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha mpaka cha Rafah kati ya eneo hilo la pwani na Misri, baada ya kivuko hicho kufunguliwa tena kwa ajili ya harakati za watu.
-
Mataifa ya Kiislamu na Kiarabu yailaani Israel kwa kukiuka usitishaji vita Gaza
Feb 02, 2026 03:41Mataifa kadhaa ya Kiislamu na Kiarabu yameulaani vikali utawala haramu wa Israel kwa kukiuka usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza
-
Hamas: Israel isitishe jinai ili mapatano ya usitishaji vita Gaza yafanikiwe
Feb 01, 2026 23:40Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa harakati za Palestina zimejitolea kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na kwamba mafanikio ya mapatano hayo sasa yanategemea kulazimishwa utawala haramu wa Israel kuyazingatia na kujiepusha na jinai inazoendeleza dhidi ya Wapalestina.
-
Wanazuoni wa Yemen watangaza mshikamano na Iran
Feb 01, 2026 23:12Jumuiya ya Wanazuoni wa Yemen imetangaza mshikamano wake kamili na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutaka ulimwengu wa Kiislamu kuchukua msimamo wa pamoja katika suala hilo.
-
Afisa wa Umoja wa Mataifa: Usitishaji mapigano Gaza si wa kweli
Feb 01, 2026 01:50Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) amelaani shambulio la jeshi la Israel katika kitongoji cha Sheikh Radwan kaskazini magharibi mwa Jiji la Gaza, ambalo limeua makumi ya Wapalestina akisema kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo hili si ya kweli.
-
Askari 10 na magaidi 109 wauawa katika mapigano kwenye jimbo la Balochistan, Pakistan
Jan 31, 2026 22:58Askari wasiopungua 10 na magaidi 109 wameuawa katika mapigano wakati vikosi vya usalama vya Pakistan vilipozima mashambulizi makubwa "yaliyoratibiwa" katika jimbo la kusini-magharibi mwa Balochistan. Hayo yalielezwa jana Jumamosi na afisa mmoja wa usalama wa Pakistan.
-
Israel yaua Wapalestina 31 wakiwemo watoto 6 katika ukiukaji mpya wa usitishaji vita Ghaza
Jan 31, 2026 11:14Wapalestina wasiopungua 31, wakiwemo kwa uchache watoto sita, wameuawa shahidi katika mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel tangu alfajiri ya leo hadi wakati huu katika Jiji la Ghaza na mji wa Khan Younis katika Ukanda wa Ghaza.
-
Kocha wa Manchester City: Mimi niko pamoja na Wapalestina
Jan 31, 2026 03:41Kocha wa timu yya soka ya Manchester City Mhispania Pep Guardiola kwa mara nyingine ametangaza himaya na uungaji mkono wake kwa Palestina na kusisitiza kwamba, yeye yuko pamoja na Wapalestina.
-
OCHA: Watu milioni moja Gaza wanahitaji makazi na msaada wa haraka
Jan 31, 2026 03:34Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu (OCHA) imeonya kwamba, hali ya kibinadamu huko Gaza bado ni mbaya, huku zaidi ya watu milioni moja wakihitaji makazi na msaada wa haraka.
-
Ripota wa Umoja wa Mataifa: Kuna ulazima wa kusitishwa uhusiano na utawala wa Israel
Jan 30, 2026 07:52Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel ametoa wito kwa nchi zote ulimwenguni kusitisha uhusiano wao na utawala wa Israel na kuweka vikwazo vya kimataifa dhidi ya utawala huo.