-
Balozi wa Yemen mjini Tehran: Tutapiga shabaha yoyote ya Marekani, Uingereza
Feb 18, 2024 22:57Balozi wa Yemen nchini Iran anasema kuwa vikosi vya jeshi la nchi yake vitashambulia vituo vyote vya Marekani na Uingereza "vinavyoweza kulengwa shabaha" kujibu mashambulizi ya hivi karibuni ya nchi hizo katika ardhi ya Yemen.
-
Afisa wa Mossad: Kila mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 4 wa Gaza ‘anastahili’ kufa kwa njaa
Feb 18, 2024 22:57Afisa wa zamani wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad, Rami Igra, amesema Wapalestina wote wa Gaza walio na umri wa zaidi ya miaka 4 wanastahili kukabiliana na sera ya adhabu jumuishi ya Israel ya kunyimwa chakula na misaada ya kibinadamu.
-
Vitisho vipya vya wakosoaji wa Natenyahu; Kuvunjwa Baraza la Mawaziri la Vita
Feb 18, 2024 06:02Sambamba na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu kuendeleza tabia yake ya kujichukulia hatua za upande mmoja, wakosoaji wake wametishia kulivunja Baraza la Mawaziri la Vita la utawala huo.
-
Afisa Mzayuni: Hatuwezi kukabiliana na mashambulizi ya Hizbullah, tunajificha tu
Feb 18, 2024 04:07Mkuu wa baraza la kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Margaliot ambaye hivi karibuni aliliomba jeshi la Israel liharibu miji ya mpakani ya Lebanon, amekiri kwamba, mashambulio ya harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ni makali mno kiasi kwamba hawawezi tena kuingia na kutoka kwa urahisi katika mji huo na kitu pekee wanachoweza kufanya ni kujificha.
-
Uhusiano wa Saudia na Syria wazidi kuimarika, Bin Salman kutembelea Damascus
Feb 18, 2024 04:06Gazeti la kimataifa la Rai Al-Youm limezungumzia kuzidi kustawi na kuimarisha uhusiano wa Riyadh na Damascus na kusema kuwa, karibuni hivi mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman atatembelea Syria ili kuzidi kuimarisha uhusiano wa opande mbili.
-
Kiongozi wa HAMAS: Israel inabeba dhima ya kukwama mazungumzo ya kusitisha vita
Feb 17, 2024 23:30Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni unawajibika kwa kushindwa kupiga hatua mazungumzo na kufikia makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.
-
HAMAS yaiasa ICJ iibebeshe dhima Israel kwa jinai za kivita Gaza
Feb 17, 2024 08:03Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iuwajibishe utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai za kivita zinazofanywa na utawala huo pandikizi dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Sayyid Nasrullah: Israel 'italipa kwa damu' mauaji ya raia wa Lebanon
Feb 17, 2024 04:40Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Israel "utalipa kwa damu" gharama ya mauaji ya hivi karibuni ya raia kusini mwa nchi hiyo, akisisitiza kwamba mauaji hayo hayawezi kuifanya harakati hiyo kuacha kuwaunga mkono na kuwatetea Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
-
Ripoti: Nchi za Kiarabu hazitaki Marekani itumie ardhi zao kuishambulia Iran
Feb 17, 2024 04:12Nchi kadhaa za Kiarabu zinaripotiwa kukataa maombi ya Marekani na washirika wake kufanya mashambulizi kutoka katika ardhi zao dhidi ya Iran na makundi ya muqawama katika eneo la Asia Magharibi wakati huu wa mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
-
Mke wa kiongozi wa Daesh (ISIS) afichua siri nzito kuhusu al Baghdadi
Feb 16, 2024 23:19Wakuu wa mahakama nchini Iraq wametangaza kuwa familia ya Abu Bakar al-Baghdadi, kiongozi wa zamani wa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) wamefanyiwa usaili baada ya kurejeshwa Iraq kutoka nje ya nchi.